MEJA JENERALI. MILANZI: ACHENI KUINGIZA MIFUGO KATIKA HIFADHI ZA TAIFA.
Rais Msataafu wa Awamu
ya Tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akizungumza mara baada ya kupokea
Matembezi kwa ajili ya kupinga ujangili ya Walk
for Elephant Dar es Salaam 2017 leo jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya
kilomita tano yameratibiwa na Asasi ya Tanzania – China Promotion Association (TCFPA)
na Ubolozi wa China ambapo yalianzia ubalozini na kuishia katika Hotel ya Sea
Cliff.
|
Na Daudi Manongi
Katibu Mkuu
Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji
kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu
uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili
unaofanywa dhidi ya Tembo
ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China
mpaka Hoteli ya Sea Cliff ambapo wageni
mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa
alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na
kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na
siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira
haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina
mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza
kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa
kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo
upigaji marufuku
biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo
mwezi machi Mwaka huu.
Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua
wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika
biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka
watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu kwani ni urithi wa kila mtanzania na
kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huu wa wanyama na
kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika kutangaza mbuga zetu na pia
kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ujangili wa pembe
za ndovu.