MBUNGE WA VITI MAALUMU CCM MKOANI MWANZA KEMIREMBE LWOTA AIPIGA TAFU HOSPITALI YA SEKOUR TOURE.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella,
akizungumza hii leo, kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 20, magodoro
20, vyandarua 20 pamoja na mashuka 100, uliotolewa na mbunge wa Viti
Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota,
katika Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure.
Na BMG
Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi, akizungumza kwenye utoaji wa msaada huo
Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo
Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzales, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Dkt.Onesmo Lwakyendera, akitoa neno la
shukurani baada ya msaada huo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella
(kushoto), akimpongeza Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoani Mwanza,
Kemirembe Lwota, baada ya kufanikisha upatikanaji wa msaada huo.
Mkuu wa mkoa wa
Mwanza, John Mongella (kushoto), akisalimiana na Mganga Mkuu mkoa wa
Mwanza, Dkt.Leonard Subi, wakazi wa kukabidhi msaada huo.
Baadhi ya akina mama wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, waliojitokeza kushuhudia zoezi hilo
Baadhi ya akina mama wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, waliojitokeza kushuhudia zoezi hilo
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mbunge viti
maalumu CCM Mkoani Mwanza, wawakilishi wa Mo Dewji Foundation pamoja na
wadau wengine, wakiwa kwenye wodi ya akina mama hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Mwanza, kujionea hali ya wodi hiyo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi, akizungumza ofisini kwake.
Baadhi ya watumishi wa afya mkoani
Mwanza, wawakilishi wa Mo Dewji Foundation, mbunge wa viti maalumu
mkoani Mwanza CCM na wanahabari, wakimsikiliza Mganga Mkuu mkoani
Mwanza, baada ya zoezi la kukabidhi msaada huo.
LakeFmHabari
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameonya juu ya suala la uchafu kukithiri kwenye wodi za wagonjwa katika vituo vya afya, zahanati na hospitali ikiwemo ya rufaa ya Sekou Toure.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameonya juu ya suala la uchafu kukithiri kwenye wodi za wagonjwa katika vituo vya afya, zahanati na hospitali ikiwemo ya rufaa ya Sekou Toure.
Mongella ametoa
onyo hilo hii leo wakati akikabidhi msaada wa vitanda, magodoro,
mashuka pamoja na vyandarua, uliotolewa na mbunge wa Viti maalumu
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota.
Ameeleza
kusikitishwa na hali ya uchafu katika wodi za wagonjwa hususani za akina
mama katika vituo vya afya, zahanati pamoja na Hospitali huku akikuta
mashuka mpya yamehifadhiwa stoo kwenye baadhi ya vituo hivyo.
“Na siyo hapa
Sekou Toure tu, hata maeneo mengine, huwa nasikitika sana ninapokuta
shuka chafu kitandani. Bahati mbaya nimewahi kwenda mahali nikakuta
shuka mpya stoo, mimi nasema hizi shuka zitumike, zichakae, tutafute
zingine”. Amesisitiza Mongella na kutaka suala la usafi kupewa
kipaumbele zaidi.
Mganga Mkuu wa
mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi, amesema huduma za afya zinaendelea
kuboreshwa licha ya kuwepo uhitaji mkubwa wa vitendea kazi ambapo kwa
siku yanahitajika mashuka manane kwa kila kitanda.
Mbunge wa Viti
Maalumu CCM Mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, amewahimiza wadau wengine
kujitokeza ili kusaidia kutatua kero za huduma za afya, huku akiishukuru
taasisi ya Mo Dewji kwa kusaidia upatikanaji wa msaada huo ambao ni
mashuka 100, vitanda 20, magodoro 20 pamoja na vyandarua 20 wenye
thamani ya shilingi Milioni 25.
Mkuu wa Taasisi
ya Mo Dewji, Barbara Gonzales, amesema taasisi hiyo imedhamiria
kusaidia uboreshaji wa huduma mbalimbali katika nyanza za elimu, afya
pamoja na maendeleo ya jamii ili kuboresha zaidi maisha ya wananchi.