Akizindua rasmi filamu ya NNDOA ZA UTOTONI kundi la Jipaze
Comeadian Group Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorius Luoga amesema kuwa Changamoto
zote zinazokabili kundi ilo zitafanyiwa kazi kwa sasa ni kundi la kwanza ambalo
limefanya suala hilo kwa lengo la kuelimisha jamii huku mkuu wa Polisi mkoa wa
kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta akitoa shilingi Millioni moja kwa ajili ya
kuwaunga mkono
Aidha kikundi hicho kilimwomba mkuu wa wilaya kuwa mlezi wao
na kuwakubalia “Hata kabla hamjasoma kwenye risala tayari nilishakuwa mlezi wa
kikundi hiki kimekuwa kikundi cha mfano lazima serikali tuwasaidie” alisema
Luoga.
|