|
Meza
kuu ikiongozwa na mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo wa halmashauri
ya Mji ndugu,Maiga Majagi aliyevaa shati ya dirafti katika katika. |
|
Msanii wa nyimbo za asili katoka kata ya Bukoli akiburudisha wakati wa mashindano hayo |
|
Meza kuu ikifatilia kwa makini kile ambacho kilikuwa kinaendelea |
|
Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Geita,Rose Bonface (ROSE BONANZA) akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa. |
|
Moja kati ya majaji katika mashindano hayo,Bi Anithar Kagemulo akijitambulisha wakati wa mashindano hayo. |
|
Kikundi cha waimbaji kutoka wilayani Chato cha Mwagazege kikiimba katika mashindano hayo. |
|
Mgeni
rasimi ambaye ni afsa maendeleo ya jamii Ndugu Maiga Majagi akizungumza
na wasanii huku akiwaasa kuendeleo kuwa na umoja na kushikamana ili
kuendeleza sanaa katika Mkoa wa Geita. |
|
Mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo ya jamii Ndugu Maiga Majagi ,akiendelea na hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mashindano. |
|
Meza kuu ikimsikiliza mgeni rasimi wakati wa hotuba yake |
|
Majaji wakifatilia mashindano |
NA MADUKAONLINE
Chama cha
wasanii Mkoani Geita,kimeiomba serikali Mkoani humo kuendelea kutoa
ushirikiano katika Nyanja hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na kusapoti
kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na wasanii.
Kauli hiyo
imesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo Rose Bonface wakati wa
ufunguzi wa mashindano ya kuwasaka wasanii wenye vipaji vya kuimba
kuigiza na kuchekesha yaliyokuwa yanafanyika katika ukumbi wa
halmashauri ya Mji wa Geita.
Rose alisema
kuwa Tasnia ya sanaa bado inachangamoto nyingi ikiwa ni pamojan na
kushindwa kutambulika na kushikwa mkono kwenye serikali kutokana na
kwamba baadhi viongozi wa kiserikali wanaona swala la wasanii limekaa
kiunu jambo ambalo si kweli kwani kazi ya sanaa ni sawa na shughuli
zingine katika jamii.
“Sisi
wasanii bado tunachangamoto kubwa sana katika serikali ingawa kwa sasa
kuna wizara inayotutambua lakini bado kuna ugumu mwingi tu tukiangali
kwenye serikali kuna viongozi ambao wanaona kuwa hatuna mchango wowote
lakini sio kweli sisi tunauwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii na
ikatuelewa zaidi kuliko vile ambavyo serikali imeendelea
kutuchukulia”alisema Rose.
Kwa upande wake mwenyekiti wa waigizaji Mkoa wa Mwanza,Ramadhani Masululi,amesema
kuwa jambo ambalo limekuwa likisababisha sanaa au wasanii kuonekana ni
wahuni ni kutokana na baadhi ya wasanii kuonekana kutokujieshimu na
wengine kuingia kwenye sanaa bila ya kuwa na maono au mtazamo chanya
katika sanaa.
“Sanaa sio
uhuni kwanini wanasema uhuni waigizaji wengine wameingia ni mamluki
unakuta mwingine anaingia kwenye sanaa ni mlevi mvuta bangi na mwingine
ni Malaya na hii ya wezekana kwasababu nikutokana na vigezo kutokuwa
vigumu lakini sisi kama chama cha wasanii hatuwezi kukubaliana na swala
hili tutaakikisha wale wenyetabia za ajabu wanatupisha ili tuwe na
wasanii ambao wananidhamu”alisema Ramadhani
Akimwakilisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita ambaye ndiye alikuwa mgeni
rasimi kwenye uzinduzi huo,afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri
hiyo,Maiga Majagi,amewaasa wasanii kutumia umoja wao kuleta mabadiliko
kwa wanageita kwa kufanya kazi na kukitumia chama chao kwa kuwa tetea
zaidi na kupata taarifa mbali mbali za soko la kazi zao na pia
amewataka kupanga mikakati ya kushirikiana na wadau wote na kwamba
jambo likiongelewa na wote linakuwa na nguvu kuliko kuzungumziwa na mtu
mmoja.