HECHE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA SERENGETI.
Ijumaa
Januari 20,2017 kumefanyika mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Serengeti inayojumuisha
mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu umefanyika katika ukumbi wa mikutano
Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Viongozi
mbalimbali wa kitaifa wa CHADEMA wamehudhuria mkutano huo ambao umeenda
sambamba na kufanya uchaguzi wa viongozi wa kanda ya Serengeti ambapo
John Heche amechaguliwa kuwa mwenyekiti,Gimbi Masaba kuwa makamu
mwenyekiti n Catherine Ruge kuwa mweka hazina.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe ametumia mkutano hiyo kutoa ujumbe kwa taifa kupitia vyombo vya habari.
Mbowe
amesema nchi ya Tanzania inapitia changamoto nyingi kwa kipindi hiki
lakini kubwa zaidi kuliko yote ni hofu inayotamalaki ndani ya taifa
kwamba watu wameanza kujiona kuwa hawako salama sana ndani ya nchi yao.
Amesema
kuna watu ambao wana hofu ya njaa,hofu ya kuporomoka kwa uchumi,hofu za
kiusalama,lakini CHADEMA ina hofu kubwa kuhusu usalama wa viongozi
wake,hofu kubwa kuhusu kutokutendewa haki viongozi wa cha hicho kuanzia
viongozi wa kitaifa,kwenda kwa wabunge,madiwani,wenyeviti wa
vijiji,wenyeviti wa mitaa hata na vitongoji pamoja na wanachama wao.
“Badala
ya kujengwa hofu ni lazima sasa tusimamie imara kuijenga CHADEMA yenye
nguvu kujenga upinzani wenye nguvu,kusimama kwa haki bila
kuogopa”,amesema Mbowe.
“Ni
juzi tu rais amemteua wabunge wengine katika orodha ya wabunge 10
anaoweza kuwateua,katiba ya nchi inasema anapaswa ateue 10,lakini kati
yao wasipungue wanawake watano,lakini hadi jana rais ameshateua wabunge
nane kati yao sita ni wanaume kwa maana hiyo tayari ameshavunja
katiba”,anasema Mbowe.
Kushoto ni mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe,katikati ni katibu
mkuu wa Chadema Vicent Mashinji na naibu katibu mkuu Chadema bara John
Mnyika wakiteta jambo wakati wa mkutano maalum wa Chadema kanda ya
Serengeti uliofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga
Wa kwanza kushoto ni Makamu mwenyekiti Chadema taifa Zanzibar,Said Issa
Mohammed.Wa kwanza kulia ni naibu katibu mkuu Chadema taifa Zanzibar
Salum Mwalim
Viongozi mbalimbali wa Chadema taifa wakiwa ukumbini
Viongozi wa Chadema wakiwa ukumbini
Viongozi wa Chadema wakiwa meza kuu
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini
Katibu mkuu wa Chadema taifa Vicent Mashinji akizungumza ukumbini ambapo
alisema vitendo mbalimbali wanavyofanyiwa viongozi wa chama hicho ni
ishara kubwa kuwa ushindi wa chama hicho umekaribia
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini
Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji akizungumza
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akitoa ujumbe kwa taifa kuhusu hali ya nchi ya Tanzania hivi sasa
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akizungumza ukumbini.Waliokaa
kushoto ni wagombea katika uchaguzi wa viongozi Chadema kanda ya
Serengeti
Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji akisoma katiba ya nchi.
Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza mwenyekiti wao
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akisisitiza jambo
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini