Na:
Lilian Lundo
Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa kiasi cha shilingi Milioni 174 kwa
kuwafanyia upasuaji wa moyo wagonjwa 6 katika
taasisi hiyo.
Hayo
yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji JKCI ambaye pia
ni Daktari Bingwa Upasuaji wa Moyo Dkt.
Bashir Nyangasa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mafanikio
yaliyotokana na upasuaji huo.
“Kwa
mwaka 2017 tumeanza kwa kufanya kambi ya kwanza ya upasuaji kwa kushirikiana na
timu ya wataalamu kutoka hospitali ya Apollo, Bangalore ya nchini India na
kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa sita (6) kati ya hao wanaume ni wanne na
wanawake wawili,” alifafanua Dkt. Nyangasa.
Aliongeza
kuwa badala ya kuwapeleka wagonjwa hao nje ya nchi, wamewaleta madaktari wa
Apollo nchini ambapo imesaidia kupunguza gharama wakati huo huo wataalamu wa
JKCI wameweza kujifunza aina mpya ya upasuaji wa magonjwa wa moyo.
Dkt.Ngangasa
alifafanua kuwa kama Serikali ingewasafirisha wagonjwa hao 6 kwenda kupata
matibabu nje ya nchi gharama ya shilingi milioni 174 ingetumika ambapo kwa
kuwafanyia wagonjwa hao hapa nchini gharama ambayo imetumika haizidi shilingi
milioni 60.
Upasuaji
uliofanyika ni upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika
mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) ambapo
upasuaji huo uliweza kufanyika bila kutumia mashine ya mapafu na moyo.
Aliongeza
kuwa upasuaji mwingine uliofanyika ni wa kubadilisha milango ya moyo (Valves)
ambayo haikuwa inapitisha damu vizuri. Pia mgonjwa mmoja amefanyiwa upasuaji wa
milango miwili ya moyo ambayo iliharibika sana, milango hiyo ilibadilishwa na kupanuliwa
kwa kishina cha mshipa mkubwa wa moyo kwa kutumia mfuko wa moyo (Aorta).
Kwa
upande wa Mshauri Mwandamizi kutoka hospitali ya Apollo Dkt. Sathyaki Nambala alisema
kuwa ni mara ya nne amekuja Tanzania, lakini kwa sasa amekuta kuna jengo jipya
kwa ajili ya wagonjwa wa moyo ambalo lina vifaa vyote muhimu na vya kisasa kwa
ajili ya upasuaji wa moyo.
Alongeza
kuwa hatua hiyo imesaidia Serikali ya Tanzania kupunguza kiasi kikubwa cha
fedha kwa kuwafanyia wagonjwa upasuaji ndani ya nchi badala ya kuwapeleka nje ya
nchi.
Vile
vile, Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo JKCI Peter Kisenge alisema kuwa Taasisi hiyo inategemea kupokea madaktari kutoka Afrika na Saudi Arabia kwa ajili ya upasuaji wa kutanua mishipa ya moyo
iliyoziba, kutanua milango ya moyo iliyoziba na kuziba matundu ya moyo.
Kambi
ya madaktari wa Afrika itakuwepo katika
Taasisi hiyo kuanzia tarehe tarehe 23 mpaka 29 mwezi huu, ambapo wagonjwa 15 watafanyiwa upasuaji wa
bila kufungua kifua(Catheterization Procedure).
Kambi
ya madaktari bingwa kutoka Saudi Arabia
watafanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Device Closure) ambapo
wagonjwa zaidi ya 55 wenye umri kuanzia miaka 12 na kuendelewa watafanyiwa
upasuaji kuanzia tarehe 04/02/2017.
Aidha
Madaktari wote nchini na wanachi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani wenye
wagonjwa wa moyo ambao wana matatizo hayo ya moyo wameombwa kuwatuma wagonjwa
katika Taasisi hiyo ili kupatiwa matibabu. Pia wanaweza kuwasiliana na Dkt.
Kisenge kuitia namba 0713 236 502 au 022-2151379.
|