Baada ya kusamba video katika mitandao ya kijamii ikionyesha
akipigwa viboko na wanaukoo Mama mmoja Mwenye umri wa miaka 38 Msimbiti na Mkulima mkazi kitongoji cha Migutu, kijijicha Kinesi
Kata ya Nyamunga Wilayani Rorya Mkoani Mara jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi
Tarime Rorya Tayari linashikilia watuhumiwa kumi kuhusiana na tukio hilo na
kati ya hao watuhumiwa watano ni viongozi wa balaza la Mila akiwemo
Mwenyekiti na wajumbe wake Wanne n
watuhumiwa wengine ni wale walioshiriki kumshika na kumlaza mhanga wa tukio hilo ili aweze kuadhibiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta
amesema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 23 Mwaka jana Majira ya saa kumi na Moja jioni katika Eneo la Mastooni lililopo kitongoji
cha Migutu, kijiji cha Kinesi Kata ya Nyamunga Wilayani Rorya Mkoani Mara,
Aidha Kamanda alisema kuwa Mtu Mmoja mwenye Umri wa miaka 38
Msimbiti Mkulima na mkazi wa kijiji cha Kinesi ambaye ni Mhanga wa tukio hilo
liliosambaa katika mitandao ya kijamii akipigwa viboko na watu sita ambapo watu hao waliamulishwa kumuchapa
viboko na wajumbe wa kumi wa baraza la mila la kabila la wasimbiti liitwalo
Irienyi ndodo baada ya kulalamikiwa na
kupelekwa katika balaza hilo baada ya kumkana mama yake mazazi mwenye
umri wa 55 huku akimtuhumu kwa uchawi.
Kutokana na mama kuripoti kwa wajumbe wa balaza ndipo
waliamulu mama huyo kupigwa viboko makalioni
hivyo mpaka saas wathumiwa kumi wanashikiliwa na jeshi la polisi
kuhusiana na tkio hilo huku wengine wakiendelea kusakwa kwa lengo la
kuwafikisha mahakamani ili kujibu suala hilo.
Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa
mahakamani mara moja kijibu shitaka linalowakabili huku jamii ikilaani vikali
unyama huo ulifanyika
|