HOSPITAL TARIME YAKUMBWA NA CHANGAMOTO YA MAJI MDAU AJITOLEA GARI LA KUSOMBA MAJI.

MWENYEKITI WA KAMATI YA UKARABATI WA HOSPITALI YA WILAYA YA TARIME PETER ZACHARIA AKIMIMINA MAJI  KWENYE NDOO BAADA YA KUTOA MSAADA WA MAJI KATIKA HOSPITAL HIYO  KWA LENGO LA KUTATUA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MAJI TAKRIBANI WIKI MOJA.
WAFANYAKAZI WA HOSPITALI WAKICHOTA MAJI

MGANGA MKUU HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME CALVIN MWASHA AKIMIMINA MAJI KWENYE NDOO BAADA YA KUPOKEA MSAADA WA GARI LA MAJI KUTOKA KWA ZACHARIA ILI KUSAIDIA KULETA MAJI HOSPIALINI HAPO KWA LENGO LA KUTATUA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MAJI KUTOKANA NA UKAME AMBAO UMESABABISHA BAADHI YA VYANZO VYA MAJI KUKAUKA NA WANACHI KUSAKA MAJI UMBALI MREFU.
MATRONI WA HOSPITALI PAULINA SHIROLE AKIMIMINA MAJI KWENYE NDOO
PETER ZACHARIA AMBAYE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA UKARABATI HOSPITALI YA WILAYA YA TARIME NA MFANYABIASHARA AKIONGEA NA CLEO NEWSTZ BAADA YA KUTOA MSAADA WA GARI LA KUSOMBA MAJI ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MAJI
MATRON WA HOSPITAL AKIONGEA NA CLEO NEWSTZ KUHUSU HADHA YA MAJI KATIKA HOSPITALI HIYO



Kutokana na ukame ambao umeashamili maeneo mbalimbali ya Nchi na kupelekea baadhi ya vyanzo vya maji kukauka  Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara imekumbwa na changamoto ya ukosefu wa maji jambo ambalo limemusukuma Mwenyekiti wa Bodi ya ukarabati wa Hospital hiyo Peter Zacharia kutoa Gari kwa ajili ya  kuleta Maji kwa lengo la kutatua changamoto hiyo.


Zacharia ambaye ni mdau wa maendeleo pia Mwenyekiti wa kamati ya ukarabati wa Hospital hiyo  na mfanyabiashara amesema kuwa ameamua kutoa msaada huo wa gari la kusomba maji ili kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika hospital hiyo kwani wagonjwa wamekuwa wakiteseka kwa sababu ya ukosefu wa maji.


 “Nikiwa tumboni mwa mama yangu na nilipozaliwa nilijaliwa na mwenyezi Mungu kuwa injinia wa mambo mbalimbali na sasa nausika na magari ya usafirishaji sasa wanachi wa Tarime ninachowalaumu hawataki maendeleo na wanapinga sana mtu ambaye anataka kuwasaidia wanachagua viongozi ambao wanajali posho na maslahi yao tu” alisema Zacharia.



Akipokea Msaada wa maji hayo Matron wa Hospital hiyo Paulina Shirole ametoa shukrani zake na kudai kuwa kipindi cha nyuma takribani wiki moja suala zima la maji limekuwa changmoto kubwa na kupelekea suala zima la usafi kukwama.

Nao baadhi ya wanachi ambao wanauguza katika Hospital hiyo wametoa shukrani zao kutokana na msaada huo huku wakizungumzia hadha waliokuwa wikipata kipindi cha Nyuma kuwa baadhi huduma zimekuiwa zikikwama kwa sababu ya ukkosefu wa maji

BAADHI YA WANANCHI WAKITOA SHUKRANI ZAO BAADA YA KUTOLEWA KWA MSAADA HUO WA MAJI

Powered by Blogger.