DIWANI NA MATENDAJI KATA WAHUKUMIWA JERA MIAKA 5 KWA KUGHUSHI NYARAKA.





DIWANI wa Kata  ya Kyangasaka   Wilayani Rorya Mustapha Sanya kichinda (Chadema) na Mtendaji wa Kata hiyo James John wamehukumiwa kwenda jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka vibaya na kughushi  nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wilaya ya Tarime Amoni Kahimba,ambapo mahakama pasipokuwa na shaka na ushahidi uliotolewa umewatia hatiani viongozi hao kwa makosa mawili likiwemo kosa la  matumizi mabaya ya Madaraka  na kutumia nyaraka kufanya udanganyifu.

Hakimu Kahimba amesema kosa la kwanza mshitakiwa namba 1.James John amehukumiwa kulipa faini sh.milioni moja au kwenda kutumikia kifungo jela miaka 2 ,ambapo kosa la pili amehukumiwa kulipa faini milioni moja na laki tano au kwenda jela miaka3.

Mshitakiwa na. 2 ambaye ni Diwani kosa la kwanza amehukumiwa kwenda Jela miaka 2 bila faini na kosa la pili mshitakiwa huyo amehukumiwa kwenda Jela miaka 3 bila kulipa faini na washitakiwa wote adhabu zao zitaenda kwa pamoja na wote wamepelekwa Gerezani.

Awali Mwendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Mara Yahaya Mwinyi amesema kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo Aprili 2013,wakati huo akiwa ni Diwani wa Kata ya Nyamagaro kabla ya kata hiyo kugawanywa ambapo kwa sasa ni Diwani wa Kata ya Kyangasaka.

Mwinyi  ameongeza kuwa Diwani akiwa kama Mwenyekiti wa WDC na mtendaji akiwa kama Katibu wa WDC  walibadilisha matokeo ya aliyekuwa mshindi nafasi ya mwakilishi mjumbe wa baraza la Katiba wilaya Juma Ally na kumpatia ambaye hakuwa mshindi  Jomo Nyamulanga .

Aidha amesema kuwa viongozi hao wote waligushi nyaraka  kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11/2007 ambapo walitumia mihitasari ya uongo na kubadilisha matokeo ya mshindi halali Ally aliyekuwa mshindi kwa kura  dhidi ya mpinzani wake Jomo aliyepata kura 1 kosa hilo lilitendeka Aprili 3/2013.


Powered by Blogger.