Mkazi wa kitongoji cha
Bondeni, kijiji cha Mpakani katika mji mdogo wa Sirari Nandi Lula (19)
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchoma kisu kaka yake, Masuke
Lula (25) na kumsababishia kifo kutokana na kuvuja damu nyingi.
Kamanda wa mkoa wa
Polisi,Tarime/Rorya Andrew Satta amedhibitisha kutokea kwa tukio hila na kusema
kuwa amesema tukio hilo lilitokea usiku wa Januari 30 kwa marehemu aliemtaja
kuwa ni Masuke Lula (25) aliyeanzisha ugomvi kwa mgodo wake Nandi Lula (19) kwa
kuchelewa kuandaa chakula na kuanza kumgombeza.
Satta ameongeza kuwa jamii inapaswa
kuwa makini na kutumia busara ili kuepusha madhara na vifo vizivyo tarajiwa
kama hiki ambacho kilitokana na kumgombeza mdogo wake hivyo kumsabaishia
apandwe hasira na kumuua kaka yake.
Shuhuda wa tukio hilo,Willison
Patrick alisema baada ya marehemu kufika
nyumbani huku amelewa alimkuta mdogo wake akikatakata nyanya kwa ajili ya
kupika mboga na kuanza kumgombeza ambo ambalo lilichochea hasira kwa mdogo wake.
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia
maiti katika Hospitali ya Mji wa Tarime, Samwel Malindi amekiri
kuupokea mwili wa marehemu na kuwa umehifadhiwa kwa ajili ya kusubiri taratibu
za maziko zifanywe na ndugu wa marehemu.
|