AKUTWA AMEJINYONGA HADI KUFA JIJINI MWANZA.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza.
MNAMO TAREHE 16.01.2016 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI KATIKA MTAA NA KATA YA NYASAKA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA ANASTAZIA FRANCIS MIAKA 48, MSUKUMA NA MKAZI WA MTAA WA NYASAKA, ALIKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFA NDANI YA CHUMBA CHAKE KWA KUTUMIA MTANDIO AMBAO ALIKUWA AMEUNING’INIZA KWENYE DIRISHA JUU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INADAIWA KUWA MAJIRA TWAJWA HAPO JUU BAADA YA MUMEWE KUONDOKA MAREHEMU ALIMTUMA MWANAE MKUBWA ALIYEMALIZA KITADO CHA NNE AENDE DUKANI NA MWINGINE MDOGO MWENYE UMRI WA MIAKA 06 AENDE KUFAGIA, AIDHA BAADA YA KUWAONDOA WATOTO WAKE INASEMEKANA NDIPO ALIPOPATA MWANYA WA KWENDA KUJINYONGA HADI KUFA. TUKIO HILO LILIJULIKANA BAADA YA MTOTO WAKE MDOGO KURUDI NDANI CHUMBANI KUCHUKUA SHATI NA KUMKUTA MAMA YAKE AKIWA AMEJINING’INIZI NDIPO ALIITA WATU ILI WAJE KUMSAIDIA.

WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO,  ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUKUTA MAMA HUYO AKIWA TAYARI AMEFARIKI DUNIA, UPELELEZI UNAENDELEA ILI KUFAHAMU CHANZO CHA TUKIO HILO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI KITENDO HICHO NI KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOPATWA NA MATATIZO WAOMBE USHAURI KWA WATU WENGINE ILI KUWEZA KUEPUSHA MAAMUZI AMBAYO NI HATARI KATIKA MAISHA YAO.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI 
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Powered by Blogger.