MSANII WA MUZIKI WA INJILI SBJ AZUA BALAA NA WIMBO WA 'YESU NIPE NYONYO',ADAIWA KUDHALILISHA DINI
Gazeti
la Kenya liitwalo taifa leo limeripoti kwamba bodi ya filamu kwenye
nchi hiyo imehuzunishwa na Msanii wa muziki wa Injili SBJ kuimba wimbo
wa Injili ambao unadhalilisha Imani.
Wimbo wenyewe unaitwa ‘Yesu nipe nyonyo‘
ambapo mkuu wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alisema baadhi ya Waimbaji wa
Kenya wamekosa maadili na kipaji cha kubuni au kutunga nyimbo nzuri
zisizochafua hali ya hewa.
Alisema wimbo huo unaendelea kukaguliwa
kwa sababu Wakenya wamekasirishwa: "Nashangaa sana mtu mzima anakaa
chini na kuimba wimbo kama huu, Wasanii wetu wamejua kuwa kama hawaongei
uchafu ama kutoa video za utata hawatasikilizwa wala kutazamwa na
wanafanya hivyo ili wapate umaarufu”
Tayari bodi hiyo ilikua kwenye mipango
ya kuwaandikia Youtube ambao ndio wanamiliki wa mtandao huo ili waiondoe
hiyo video kwasababu bodi hiyo inayo mamlaka na katiba haitakubali
Wasanii kutunga nyimbo za kudhalilisha imani.