MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AAHIDI KUTEKELEZA MKAKATI WA SERIKALI KWA WAKATI.
Waziri Mwakyembe (kushoto) akiwa na RC Makonda (kulia).
Na James Salvatory, BMG DarMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemuahidi Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Harison Mwakyembe kutekeleza kwa wakati mkakati wa serikali wa kujenga mahakama za mwanzo 20 kwa kila wilaya ili kuchochea upatikanaji wa haki kwa haraka zaidi.
Jana Dkt.Mwakyembe alimtembelea Makonda na kumpongeza kwa juhudi zake mbalimbali anazozionesha katika uongozi wake ikiwemo utafutaji wa vijana wanasheria 35 ambao watakuwa wakitoa msaada wa kisheria bure katika mkoa wa Dar es salaa.
Waziri Mwakye alisema atatoa ushirikiano wa kutosha huku akiwataka wakuu wa wilaya na mikoa ambao ndiyo wenyeviti wa kusimamia maadili katika mahakama kufanya kazi hiyo ipasavyo kwa kuunda kamati za maadili na kuwaripoti wale wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi zao
Ujenzi wa mahakama 20 za mwanzo umekuja baada ya kuanza kwa ujenzi wa vituo 20 vya polisi kwa mkoa huo ambapo kila wilaya itakuwa na vituo vinne.