KINARA WA MASHAIRI KUJULIKANA HII LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Na James Salvatory BMG Dar
Mashindano ya kumsaka kinara wa Mashairi pamoja na Utunzi yameanza jana Jijini Dar es salaam na yanategemea kufiki tamati leo.

Mashindano hayo yamelenga kuuenzi mchango wa Meya wa kwanza barani Afrika ambaye pia alikuwa mshairi, Abeid Amiri Kaluta, lakini pia kuitumia sanaa hiyo kujadili changamoto na maendeleo ya Jiji la Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Mashindano hayo, Chata Michael, amesema washindi watatangazwa leo ambapo wa kwanza atapata zawadi ya fedha taslimu laki tano, wa pili laki tatu na wa tatu laki mbili.

Amesema licha ya mashindano hayo kuibua vipaji, pia yamelenga kuikuza taaluma hiyo sambamba na wanataaluma wake kujitambua na kuitumia sanaa hiyo kuienzi lugha ya Kiswahili na washairi watakaofanya vizuri watatumiwa kutengeneza vitabu vya ushairi vitakavyotumika katika shule za hapa nchini.

Mashindano hayo yameandaliwa na Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, ambapo yamejumuisha washairi 30, yatakuwa ni ya muendelezo na mambo yakiwa vizuri hapo baadae  yatahusisha mikoa yote nchini.
Powered by Blogger.