WANAWAKE MKOANI MWANZA WATAKIWA KUHUDHURIA KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Wanawake mkoani
Mwanza wamehimizwa kuhudhuria Kongamano la Sauti ya Mwanamke
litakalowakutanisha baadhi ya wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini,
ili kujifunza na kuhamasika katika kujikwamua kiuchumi.
Mwandaaji wa
Kongamano hilo, Mboni Masimba ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha
runinga cha The Mboni Show, amesema kongamano hilo limelenga
kuwahamasisha wanawake kufanya kazi kwa bidii na kwa kujiamini zaidi
bila kuongopa vikwazo vya kibiashara.
“Njoo ujifunze
nguvu ya mwanamke katika biashara, kushinda vikwazo, kujiamini, kufanya
kazi kwa bidii, kutoogopa hatari za kibiashara pamoja na kuwa na malengo
ya muda mrefu ambapo wahamasishaji na wafundaji mbalimbali watakuwepo”.
Amesema Masimba na kuongeza kwamba pia kutakuwa na burudani ya muziki
kutoka kwa Isha Mashauzi na Zarry Edosha pamoja na vichekesho kutoka kwa
Katarina Wa Karatu.
Aidha Masimba
amesema tayari tiketi za kongamano hilo litakalofanyika tarehe sita
mwezi huu kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza zimeanza
kuuzwa kwa shilingi elfu arobaini katika maeneo mbalimbali ikiwemo Gold
Crest Hotel, TSN Super Market Rock City Mall, Flora Salon, Kayvies Beaty
Parlour Magnum Hotel Ghana, Idda Garments Ghana, Diamond Bar Kona ya
Bwiru pamoja Bladict Classic Wear mtaa wa Uhuru Dampo.
