Miaka kadhaa
iliyopita kabla ya matumizi ya tekinolojia kuingia na kushika kasi mtu
ulikuwa ukitaka kusafiri itakubidi kuulizia kwa watu ambao tayari
wameshawahi kuwepo kwenye eneo unalolitarajia kwenda.
Baadae kidogo
simu zilivyoanza kuingia zilirahisisha mambo watu wakawa wanapigiana
simu na kuulizana hali na mazingira kwa ujumla ya eneo wanalotaka kwenda
ili kujiandaa vema.
Lakini sasa
hivi kwa msaada wa tekinolojia ni wewe tu aidha na simu au kompyuta yako
iliyounganishwa vizuri na mtandao wa intaneti ambapo unaweza kupata
taarifa lukuki bila ya kumuhusisha mtu yeyote yule.
Kadiri ya
maendeleo ya tekinolojia yanavyokua sehemu mbalimbali duniani na ndivyo
huduma mbalimbali zinavyosogezwa na kurahisishwa zaidi kumzunguka
binadamu.
Leo hii mtu
huna haja ya kupata shida ya kuanza kusumbuka kutembea umbali mrefu au
kumuuliza jirani, ndugu au jamaa kuhusu huduma kama vile za usafiri,
malazi, bidhaa, na bei zake kwani kila kitu kimo na kinaweza kupatikana
kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Vivyo hivyo kwa
upande wa huduma za usafiri na utalii zilivyorahisishwa na mitandao ya
huduma za hoteli kama vile Jumia Travel, Expedia, Airbnb, TripAdvisor,
Booking.com na kadhalika.
Wasafiri na
watalii wengi wa siku hizi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi
wanapenda kupata huduma wazitakazo kwa urahisi zaidi na uhakika wakiwa
mahali popote.
Wanataka kwamba
wakiingia kwenye mtandao aweze kupata taarifa zote juu ya sehemu
anayotaka kwenda kama vile atafika kwa njia gani pamoja na sehemu
atakayofikia.
Kwa upande wa
malazi mitandao iliyotajwa hapo juu imekuwa na nafasi kubwa sana katika
kuhakikisha msafiri anapata sehemu ya uhakika anayoihitaji, gharama na
hadhi yake.
Mitandao hii inatoa uwanja mpana wa kuweza kupata huduma zote sehemu moja, za uhakika tena ndani ya muda anaoutaka msafiri.
Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo ilimbidi mtu afanye taratibu za malazi kwa sehemu anayokwenda mpaka atakapofika.
Kwa namna moja
ama nyingine mitandao hii ya huduma za hoteli kwa mtandao na tekinolojia
kwa ujumla imeleta msaada mkubwa na mapinduzi ya hali ya juu kwa watoa
huduma nchini na sehemu zingine duniani.
Licha ya
maendeleo hayo na madhumuni mazuri ya tekinolojia katika kuboresha
maisha ya binadamu lakini bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji
hususani wasafiri kuiamini na kuitumia mara kwa mara lakini pia hata kwa
wenye hoteli na sehemu zingine zinazotoa huduma za malazi kwa ujumla.
Bado wasafiri
wengi wanaamini kuwa huduma za kweli na uhakika utazipata mara
utakapofika eneo husika licha ya kuwa kwenye mitandao hii kuna picha,
huduma, gharama na mawasiliano ya wahusika.
Na kwa upande
wa wamiliki wa sehemu za malazi kama vile hoteli bado nao hawana imani
kubwa na wamiliki wa hii mitandao. Wao wanadhani kwamba wanaweza kutumia
hoteli zao kuwatapeli wateja na kunufaika wao binafsi, dhana ambayo si
kweli.
Ukweli wa mambo
ni kwamba kwa watumiaji wa huduma hizi, wateja na wamiliki wa hoteli
ambao huitumia mara kwa mara wamethibitisha imekuwa na msaada mkubwa
sana.
Kwa mfano,
hoteli nyingi hutegemea umaarufu wa sehemu husika ndio mteja aende na
kutumia huduma zao kitu ambacho kwa dunia tuliyopo na tunayokwenda nayo
kinapitwa na wakati.
Kupitia
mitandao hii wamiliki wa hoteli na sehemu zingine za malazi wana wigo
mpana wa kuwapata wateja kutoka maeneo mbalimbali kwani huduma zao
zinakuwa tayari kwenye mitandao hiyo.
Jumia Travel ni
miongoni mwa mitandao hiyo ambayo inayo orodha ndefu ya hoteli
takribani 1,500 za nchini Tanzania bara na visiwani ambazo zinaweza
kufikiwa na watu wa ndani na nje ya nchi.
Hii ni fursa
kwa wamiliki wa hoteli kuweza kutambua wateja wao ni watu wa aina gani
na wanatarajia vitu gani kutoka kwao. Wateja wa sasa wanategemea kwa
kiasi kikubwa kukuta taarifa zote kuhusu huduma za hoteli husika kuwepo
kwenye mtandao na kupatikana mara moja pale wanapozihitaji.
Kwa bahati
mbaya si hoteli na sehemu za malazi zote ambazo taarifa zake unaweza
kuzikuta mtandaoni na hapo ndipo mitandao hii inapokuja kuziba hilo
pengo.
Mitandao ya
huduma za hoteli imekuja kuziba pengo lililokuwepo kwa muda mrefu baina
ya watoa huduma hizo na wateja ambapo athari zilikuwa kwa pande zote
mbili.
Wamiliki kwa
kiasi kikubwa wamekuwa wakikosa wateja wengi ambao wangeweza kuwafikia
kwa njia ya mtandao kwa kutegemea ambao wanakwenda moja kwa moja na
hivyo kupoteza mapato mengi. Na pia kwa wateja ambao walikuwa na shauku
ya kujua sehemu husika kabla ya kwenda walikuwa wanakosa fursa hiyo kwa
sababu hakukuwa na mbadala wa huduma hiyo.
Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel
(travel.jumia.com) ni mtandao nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli
kwa njia ya mtandao wenye orodha ya hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za
Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.
Dhumuni letu ni
kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na
kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.
Hapa Jumia
Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao
huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi
zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan
(Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda),
Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto
(Ureno) na Paris (Ufaransa).
Kabla ya mwezi
Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago.
Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na
MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas kama washirika wao katika
masuala ya kifedha.
Imeandaliwa na Jumia Travel Tanzania |