UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi
Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mkurugenzi wa
Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha
Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo, Dar es Salaam leo
asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku
saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto),
akizungumza na wajumbe hao.
Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.
Na Dotto Mwaibale
UJUMBE wa watu
sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa
ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM)
Akizungumza na
waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani
Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya
Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa
chama hicho, Jia Bo.
Madabida
alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina
ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa
Taifa hilo Hayati Mao Tse-Tung.
Alisema ujumbe
huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini
kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China
ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua
kama wameyafanyia kazi.
Mratibu wa
Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni
matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.
" Ujio wa
wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi
nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba, Ulaya hasa katika
siasa za kijamaa" alisema Chana.
Alisema wenzetu
wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo
mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu
na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.