TAKUKURU YAANZA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WABUNGE WA CCM KUHONGWA MILIONI 10 KILA MMOJA
Tuhuma hizo zilitolewa
wiki iliyopita Bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman
Mbowe alipomuuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Hata hivyo, swali lake halikupata jibu ndani ya jengo hilo baada ya kuwekewa zuio na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alieleza kuwa halikuwa swali la kisera.
Hata hivyo, swali lake halikupata jibu ndani ya jengo hilo baada ya kuwekewa zuio na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alieleza kuwa halikuwa swali la kisera.
Mbowe
alitaka kufahamu kutoka kwa Waziri Mkuu kama tuhuma hizo ni za kweli au
la, akidai fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuwashawishi kupitisha
muswada wa sheria ya huduma za habari na mpango wa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema kuwa taasisi hiyo imeanza
uchunguzi kama alivyosema Rais John Magufuli alipokuwa akijibu swali
katika mkutano wake na vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita,
Ikulu jijini Dar es Salaa.
“Ndiyo, tumeanza kuchunguza, Takukuru ni chombo chake na tumeanza kazi hiyo,” Mlowola anakaririwa .
Mkuu huyo wa Takukuru alifungua mlango kwa yeyote mwenye ushahidi kuhusu tuhuma hizo aziwasilishe ili kukisaidia chombo hicho.