SHIRIKA LA WOTESAWA LATAMBULISHA MRADI WAKE WA SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI.
Mkurugenzi wa
Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTE SAWA
lililopo Jijini Mwanza, Angela Benedicto, akizungumza hii leo wakati wa
kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI"
utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana
Jijini Mwanza.
Na BMG
Benedicto amesema Mradi wa Sauti ya
Watoto Wafanyakazi wa nyumbani umelenga kuhamasisha jamii kuondoa aina
zote za unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani
ambapo wanajamii watajengewa uelewa juu ya vitendo vyote vya
unyanyasaji na unyonyaji vinavyomuathiri mtoto mfanyakazi wa nyumbani
ili kushiriki katika kuvitokomeza.
Aidha ameongeza kwamba mradi huo
utaongeza ushiriki wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani katika kujilinda
dhidi ya aina zote za unyanyasaji na unyonyaji ambapo unaambatana na
ujumbe usemao "Saidia kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyonyaji dhidi
ya watoto wafanyakazi wa nyumbani".
Katika mradi
huo ambao ni wa muda wa miezi sita, wananchi wataweza kutoa taarifa za
ukatili na unyanyasi kwa watoto wafanyakazi wa nyumba kwa kupiga simu
nambari 0800 71 00 60 bure kabisa.
Wadau
waliohudhuria kwenye utambulisho wa mradi huo ni pamoja na Madiwani,
Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa mitaa, maafisa maendeleo ya
jamii, waajiri wa watoto wa nyumbani, watoto waajiriwa wa nyumbani,
mawakili, maafisa kazi, maafisa elimu kata, wawakilishi wa dawati la
jinsia kutoka vyombo vya ulinzi pamoja na kamati za ulinzi na usalama wa
mtoto ambapo wameahidi kutoa ushirikiano wao ipasavyo ili kufikia
malengo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za
Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTE SAWA lililopo Jijini Mwanza, Angela
Benedicto, akizungumza hii leo wakati wa kutambulisha mradi wa "SAUTI
YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za
Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Zubeda Kimaro, akifungua mkutano wa kutambulisha mradi wa
"SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata
za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Amelipongeza shirika la WOTESAWA kwa
kazi nzuri ya kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani na
kuhakikisha kwamba ukatili dhidi yao unatokomezwa kabisa.
Washiriki wa mkutano wa utambulisho wa
Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani wakimsikiliza
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Zubeda Kimaro, wakati
akifungua mkutano huo.
Jaqueline Ngalo ambaye ni Mwanasheria kutoka shirika la WOTESAWA akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa
kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI"
utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana
Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa
kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI"
utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana
Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa
kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI"
utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana
Jijini Mwanza.
Miradi ya Shirika la WOTESAWA
Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani umefadhiriwa na Taasisi ya The Foundation For Civil Society.