Picha 20: WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPEWA ELIMU YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO
Hapa
ni katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga
Press Club- SPC) ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga
limekutana na waandishi wa habari na kuwapatia elimu kuhusu namna ya
kukabiliana na majanga ya moto.
Elimu hiyo imetolewa na Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi Msaidizi Benjamin Kinenge aliyekuwa
ameambatana na Afisa Habari wa jeshi hilo wilaya ya Shinyanga Felix
Banzi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Kinenge alisema miongoni mwa
majukumu ya jeshi hilo ni kuzima moto ili kuokoa maisha na mali za raia
na kuhakikisha hakuna madhara yanayoweza kujitokeza.
“Ili kutekeleza majukumu yetu tunahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali
wakiwemo wananchi ndiyo maana tunaendelea kutoa elimu katika makundi
mbalimbali kuhusu namna ya kukabiliana na majanga ya moto”,alisema
Kinenge.
Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi hilo pindi panapotekea tukio
lolote la dharura kama vile ajali za vyombo vya usafiri,moto katika
majengo,kutumbukia chooni,kisimani,kwenye bwawa,kufukiwa na kifusi na
matukio mengine.
“Kama kuna tukio toa taarifa mapema kwa jeshi la uokoaji mkoa wa Shinyanga kupitia namba zifuatazo Bure (Vodacom na Tigo) namba 114,zingine ni TTCL 028 2762600,Tigo 0679542351 na Vodacom 0752565490,pigeni simu katika namba hizi mapema ili tuwahi eneo la tukio ili tuweze kuzima moto na kufanya uokoaji kwa haraka zaidi”,alifafanua.
Kwa upande wake katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga Stephen Wang’anyi alilishukuru jeshi hilo kwa kuona umuhimu wa
kukutana na waandishi wa habari na kuwapa elimu kuhusu namna ya
kukabiliana na majanga ya moto majumbani na katika ofisi.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuliomba jeshi hilo kufikisha elimu kwa
wananchi wengi zaidi sambamba na kusambaza namba za mawasiliano
zinazotumika wakati wa matukio ya dharura ili wananchi waweze kutoa
taarifa kwa jeshi hilo wakati yanapojitokeza matukio.
Angalia picha hapa chini matukio yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo
Hapa ni ndani ya ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
SPC- ,Kushoto ni mwenyekiti wa SPC,Kadama Malunde,katikati ni Afisa
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi
Msaidizi Benjamin Kinenge ,kulia ni Afisa Habari wa jeshi hilo wilaya ya
Shinyanga Felix Banzi .Picha zote na Suleiman Abeid- Malunde1 blog
Waandishi wa habari wakiwa ofisini na maafisa kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga
Kulia ni Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya
Shinyanga,Mkaguzi Msaidizi Benjamin Kinenge akitoa elimu kwa waandishi
wa habari kuhusu namna ya kukabiliana na majanga ya moto.Kushoto ni
mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu
Mafunzo yanaendelea
Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi
Msaidizi Benjamin Kinenge akielezea somo la moto/sayansi ya moto
Mafunzo yanaendelea
Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi
Msaidizi Benjamin Kinenge akionesha kimiminika kinachotumika kuzimamoto
Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi
Msaidizi Benjamin Kinenge akifundisha kwa vitendo somo la moto na namna
ya kuzima moto Fire Extinguisher
Afisa Habari wa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Felix
Banzi akionesha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa kutumia Fire
Extinguisher
Waandishi wa habari wakiangalia moto
Moto unawaka
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja,Jenifer Paul Mahesa akizima moto kwa kutumia Fire Extinguisher
Waandishi wa habari wakiendelea kupata elimu kutoka kwa maafisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stephen Wang’anyi akizima moto
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stephen Wang’anyi akiendelea kuzima moto
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akizima moto
Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi
Msaidizi Benjamin Kinenge akiendelea kutoa elimu ya sayansi ya moto
Waandishi wa habari wakifuatilia somo
Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi Msaidizi Benjamin Kinenge akielezea
umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto majumbani na ofisini.
Picha zote na Suleiman Abeid- Malunde1 blog