Mambo 5 Makubwa aliyofanya Rais Magufuli Ndani ya Mwaka 1.

Ikiwa ni mwaka mmoja wa Rais John Magufuli madarakani kuna mambo mbalimbali ameyafanya yanaweza kutajwa kuwa yametikisa Taifa katika utawala wake.
Mambo hayo kati ya mengi yamelitetemesha Taifa kwa nyajati tofauti kutokana na kasi ya Rais Magufuli kiutendaji, huku baadhi ya watu wakifurahia hatua hizo na wengine kuumia na kunung’unika kwa kuguswa katika maeneo yao ya utendaji.
Kufuta safari za nje, kufuta sherehe za kimataifa, kutangaza serikali kuhamia Dodoma, kuondoa watumishi hewa, elimu bure.
Kuzuia mikutano ya siasa kutumbua watendaji wa serikali na taasisi zake na zile za umma.
  1. WATUMISHI HEWA-alitangaza mpango wa kuondoa watumishi hewa siku ya
    maadhimisho ya wafanyakazi,alibainisha watumishi hewa 10,295 serikalini kati yao watumishi hewa 8,373 wametoka Tamisemi na 1,922 wanatoka serikali kuu
  2. KUFUTA SHEREHE-Novemba 8 mwaka jana, ikiwa siku 3 baada ya kuapishwa alitangaza kuokoa sh. Milioni 225 zilizochangwa kugharamia hafla ya wabunge na kuagiza zinunulie vitanda kwa ajili ya hospital ya Taifa Muhimbili.
  3. KUFUTA SAFARI ZA NJE-Novemba 7 mwaka jana Rais alitangaza kufuta safari za nje ya nchi kwa viongozi wa serikali, wa ngazi zote hadi mawaziri, watakaosafiri kwa kibali maalumu.
  4. KUHAMIA DODOMA-Rais Magufuli alitoa kauli ya kutaka serikali kuhamia Dodoma huku akisisitiza atahakikisha serikali yote inahamia mkoani humo kufikia mwaka 2020.
5.KUHAMIA DODOMAAFUFUA SHIRIKA LA ATCL-kwa kununua ndege mbili mpya
Powered by Blogger.