Ili kuendelea kupambana na suala zima la uvuvi haramu mkuu
wa wilaya ya Rorya Simon Chacha ameteketeza zana haramu zenye thamani ya ya zaidi ya shilingi Millioni 69 yakiwemo
makokoro ya Sangara 64, Nyavu za Timba281,Nyavu za dagaa30 na Nyavu za kuzamia
8 katika Mwalo wa Nyang,abo Kata
Nyamagaro Wilayani rorya mkoani Mara
Aidha baada aya kuteketeza zana hizo mkuu wa wilaya huyo
alielekea katika kituo cha polisi Marini Sota na kuteketeza tena Kokoro za
Sangara 46,Timba 879,Na Nyavu za dagaa 27 lengo ni kuhakikikisha Sereikali
inatokomeza uvuvi haramu ambao unaendelea katika maeneo mbalimbali katika Ziwa
Victoria.