MKUU WA MKOA MARA AMASISHENI WANANCHI KUJIUNGA NA MIFUKO YA BIMA YA AFYA
| WAHUDUMU WA AFYA WAKISIKILIZA MKUU WA MKOA WA MARA |
Mkuu wa mkoa wa Mara Charles Mlingwa amewataka Viongozi wa serikali
na na watendaji wa Vijiji na Kata kuendelea kuamasisha wananchi kujiunga na
mfuko wa Bima ya Afya ili kuweza kupata matibabu huku wakiunganisha familia zao
kwa lengo la kuwapunguzia mlolongo wa kulipa fedha nyingi pale wanapohitaji
huduma ya Afya katika Hospitali.
Hayo yamebainishwa kipindi mkuu wa mkoa huyo akiongia na
Wahudumu wa Afya Hospitali ya Halmashuri ya mji wa Tarime Mkoani Mara huku
akiwataka watumishi hao kuendelea kuwa na maadili ya kazi na kuboresha utendaji
kazi kwa lengo la kuletea wananchi maendeleo.
Mlingwa alisema kuwa endapo wananchi wataweza kjiunga katika
mifuko ya bima ya Afya itawasaidia kuhakikishia wanapata Huduma ya Afya mahali
popotea bila ya usumbufu.
Aidha mkuu wa mkoa alisema kuwa serikali tayari imejipanga
kwa lengo la kuendelea kutatua changamoto zinazokabilia idara ya Afya zikiwemo
sare pamoja na upungufu wa madawa katika Hospitali za serikali.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amezidi kuwataka wahudumu wa Afya
kuendelea kuwa wazalendo kwa kuwahudumia
wananchi vizuri huku wakiondokana na visingizio
huku wakitumia kauli ya Hapa kazi tu kwa vitendo na kuchukua hatua kwa
spidi huku wakitumia utalaamu wao kwani mgonjwa anahitaji huruma kwani serikali
inatambua uwepo wao.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo ameweza kuzungumzia mikakati
aliyonayo kuhakikisha anatatua changamoto ya Maji safi na salama mbali na kuwa
karibu na Ziwa Victoria ambapo alisema
kuwa hivi karibuni anatarajia kuwa na kikao cha wadau ili kuzungumzia suala
zima la maji.
Hata hivyo Mlingwa amezidi kumpongeza mkuu wa wilaya ya
Tarime Glorious Luoga kuendelea kusimamia suala zima la Amani ikiwemo
uboreshaji sekta ya Afya pamoja na usimamizi wa kutekekteza madawa ya kulevya Bangi ambazo zinalimwa na
wananchi ikiwa ni pamoja na kuendelea kusimamia vyema suala zima la Amani.
![]() |
| WAKITEMBELEA MAZINGIRA YA HOSPITALI HALMSHAURI YA MJI WA TARIME |

