HALMASHAURI YATOA MILLIONI MOJA LAKI NNE KWA WAHANGA WA MOTO
| WAHANGA WAKISILILIZA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME YOMAM |
Halmashauri ya wilaya
ya Tarime mkoani Mara imetoa shilingi millioni moja na laki Nne kwa kaya 11
zilizoathilika na suala la kuungua Nyumba 15 katika kitongoji cha Nyabikondo
kijiji cha Kewanja kata ya Kembambo Nyamongo Wilayani Tarime mkoani Mara ili
wanachi waweze kumalizia ujenzi wa
Nyumba hizo ili kuondokana na hadha ya Mvua ambazo zimeanza kunyesha
Wakipokea fedha hizo
kutoka kwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa Yomani
wananchi hao wamezidi kutoa shukrani kwa serikali kwa kuona umhimu wa kutoa
fedha hizo ili ziweze kuwasaidia
“Kuna baadhi ya kaya
zetu ziliweza kuungaua na kila kitu kuungua ndani zikiwemo Sare za shule za
wanafunzi sasa hii fedha itasaidia ka kiasi kikubwa kuweza kununua mahitaji
muhimu baadhi yetu tutamalizia ujenzi ili kuepukana na Mvua ambazo zimeanza
kunyesha” walisema Wananchi.
Akikabidhi Fedha hizo
kwa wahanga wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa
alisema kuwa suala hilo limepatiwa
ufumbuzi baada ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na mkurugennzi kutembelea
maeneo hayo na kutoa fedha hizo ili kuwasaidia kumalizia ujenzi.
Misiwa alisema kuwa Halmashauri imekaa na kuona kutumia
vyanzo vya mapato ya Ndani ili kuweza kutoa kiasi hichi cha fedha kwa lengo la
kuwasaidia wanachi ambao waliweza kuathilika na moto ambao ulikuwa ukichoma
Nyumba hivyo bila kujua chanzo chake katika kitongoji cha Nyabikondo na Kemambo
Nyamongo.
Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Kewanja Sumun Samson amesema kuwa suala hilo la nyumba kuungua
zenyewe lilichukua takribani Tangu
septemba Tano mpaka kumi na tatu siku sita
bila kupatiwa ufumbuzi huku zikungua jumla ya Nyumba 15 katika kaya 11
hadi sasa suala hilo limeisha huku akizidi kuwaomba wanachi kuendelez
ushirikiano ili kudumisga suala la amani
Naye Kaimu Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Tarime Peter Nyanja alisema kuwa fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya
kutimiza ahadi iliyohaidiwa na Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tarime
Glorious Luoga baada ya kuwatemmbelea wahanga hao.
Zabron mrimi ni katibu
wa Mbunge jimbo la Tarime vijiji alisema kuwa suala la kuungua kwa nyumba hizo
watoto wawili wa Familia moja waliweza
walipata majeraha ya moto na mpaka sasa hali zao ni Nzuri ambapo ofisi ya
mbunge iliweza kutoa msaada wa godoro tano pamoja na Mchele kwani baadhi yao
vyakula viliweza kuungua ndani
| MTENDAJI WA KJIJI CHA KEWANJA SUMUN SAMSON AKIONGEA NA WAHANGA WA MATUKIO NYAMONGO |