MCHUNGAJI KULOLA ARINDIMA KWENYE HITIMISHO LA MKUTANO MKUWA WA INJILI KANISA LA EAGT POSTA B MABATINI JIJINI MWANZA.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT
Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses
Kulola (pichani), kwa siku tatu mfululizo hadi jana jumapili Oktoba 16,
2016 alihudumu katika Kilele cha Mkutano Mkubwa wa Injili uliofanyika
Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, uliofanyika kwa juma
zima kuanzia Oktoba 09 hadi Oktoba 16 mwaka huu.
Ulikuwa Mkutano uliojaa Neema ya
Mungu ambapo makumi kwa mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza, walimgeukia
Kristo na kuokoka huku waimbaji mbalimbali ikiwemo Kwaya ya Havillah,
Mwanyamaka, Emmanuel Mgogo, Elineema Babu pamoja na waimbaji wengine
wengi wakihudumu katika mkutano huo.
Mchungaji Kulola aliwahimiza wakristo
kuweka dini zao pembeni na kumtumikia Mungu kwa roho na kweli huku
wakiacha tabia ya kumuonea Kristo aibu.
"Tujivunie maamuzi tuliyonayo ya
kuokoka maana hatukufanya makosa na kwa kuwa tunaye Yesu Kristo ambaye
neno lake linakatakata kama upanga naomba wote tuwe vichaa kwa ajili
yake". Alisisitiza Mchungaji Kulola akiwataka waliokoka kumtumikia Mungu
bila hofu yoyote.
Na BMG
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu katika mkutano huo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu katika mkutano huo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, Lameck Nkumba, akiomba kwenye Mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo Mchungaji wa Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, Lameck Nkumba (kulia).
Waumini wakifuatilia mkutano huo
Baadhi ya waumini wakifuatilia mkutano huo
Waumini wakifuatilia mkutano huo