KASI YA UJENZI WA MAKAZI HOLELA MILIMANI KATIKA JIJI LA MWANZA NA ATHARI ZAKE.
Serikali kupitia kwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, imetangaza zoezi la
kurasimisha makazi yaliyojengwa kiholela katika maeneo ambayo yalikuwa
hayajapimwa na kutoa hati ya umiliki kwa wamiliki wa makazi hayo ili
waweze kutambulika na kuzitumia hati hizo katika taasisi za kifedha
kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao.
Hata hivyo zoezi hilo halitawahusu
wakazi walio kwenye maeneo hatarishi ikiwemo mabondeni, milimani na
hifadhi za barabara na tayari mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni
Kibamba, amepiga marufuku ujenzi katika maeneo hayo kuendelea.
Pichani ni makazi yaliyojengwa
kiholela katika moja ya maeneo hatarishi (milimani) eneo la Mabatini
Jijini Mwanza na unaambiwa miaka ya 1980 hakukuwa na nyumba hata moja
katika eneo hilo hivyo serikali ilipuuzia kasi ya ujenzi katika maeneo
ya aina hiyo na sasa madhara yake yamekuwa makubwa ikiwemo vifo kutokana
na baadhi ya nyumba kuporomokewa na mawe pamoja na utiririshaji wa
vinyesi wakati wa mvua na hivyo kusababisha magonjwa ya miripuko ikiwemo
kipindupindu.
JICHO LA BMG