FAST JET YAANZISHA SAFARI ZA NDEGE MPYA NCHINI. WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.
| Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo. |
| Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Christina Kausan. |
|
Wanahabari
wakichukua taarifa hiyo.
|
WANANCHI
wametakiwa kuchangamkia usafiri wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya
kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu
zaidi kwa matumizi.
Mwito
huo umetolewa na Dar es Salaam leo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John
Corse wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahisi
kwa matumizi ya usafiri hapa nchini.
Alisema
kuwa ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 108 aliongeza kuwa zitahudumia
kwa miezi 6 huku ikitoa nafasi kwa mafunzo wa marubani wa Fast jet hapa nchini.
Aliongeza
kuwa kwa kuwa Fast jet hapa nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo ndege hizo
kwa kuwa hazitumii matufa mengi itasaidia kuiimarisha biashara.
"
Hii imetokea tu kuwa wakati serikali imeleta aina ya ndege zisizotumia mafuta
mengi na sisi tulikuwa pia tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa sasa binafsi
naona kuwa watanzania watanufaika zaidi" alisema Corse.
Pia
aliipongeza serikali kwa kuleta ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400 ambazo
zinaenda mikoa ya Rukwa, Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za Fast jet
hazifiki.