|
Baada ya kuendelea kutokea kwa
matukio ya kulipuka kwa moto na kuunguza nyumba za wananchi katika kitongoji
cha Nyabikondo kijiji cha kewanja kata ya Kemambo Nyamongo Wilayani Tarime
Mkoani Mara wananchi wameimba serikali kutoa msaada wa haraka ili kunusuru
wahanga hao huku viongozi wa dini kupitia madhehebu yote kuingilia kati ili
kutoa msaada wa kiroho ili suala hilo la kuungua kwa moto kijijini hapo liweze
kuisha mara moja.
Hayo yamebainishwa na wanachi katika
mkutano wa kijiji uliofanyika kijiji cha Kewanja Nyamongo juu ya kujadili suala
zima la kuungua kwa Nyumba ambapo sasa zimeisha ungua Nyumba 14 zikiwemo za
nyasi 11 na za bati 4 huku watoto Wanne wakijeruhiwa kwa moto jambo ambalo
limewanyima amani wanachi hao na kupelekea kulala nje kwa kuhofia moto huo.
Nicodemus Keraryo ni mmoja wa wanachi
akitoa maoni katika mkutano huo kuhusu suala zima la kulipuka kwa moto alisema
kuwa viongozi wa dini kupitia madhehebu yote hawana budi kuingilia kati kwa
ajili ya kutoa maombi ili suala hilo kumalizika.
“Watu tunapaswa kufunga toba na kushirikiana
na viongozi wa dini kijijini hapa na kuweka kambi katika kitongoji ambacho
kimeathilika sana ili kuombea wahanga wa matukio na mwenyezi mungu atasikiliza
kilio chetu" Alisema Keraryo.
Tanzania Omutima ni Mwenyekiti wa
kijiji cha Kewanja amezidi kuwasihi
wanachi kuendelea kutoa taarifa ili kuweza kubaini chanzo cha Moto huo huku
akiwakikishia suala zima la ulinzi na usalama na kuaidi kuendelea kushirikiana
na jeshi la polisi katika kukomesha suala hilo.
“Wananchi endeleeni kuchukua taadhali
kubwa sana juu ya matukio haya ambayo yanazidi kutushangaza wakazi wote wa
Kewanja” alisema Omutima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Nyabikondo Nelson Nyangi amesema
kuwa mpaka sasa tayari zimeungua Nyumba 14 hivyo ameiomba serikali kutoa msaada
wa haraka ili kuokoa watoto wadogo wanaolazwa nje,
Morris Okinda ni Ocd Kituo cha
Polisi Nyamwaga amlisema kuwa suala la
kuchoma Nyumba mchana ni kosa kubwa sawa na mauaji na jeshi la polisi halitafumbia macho jambo hilo huku akilaani vikali wanganga wa
kinyeji ambapo kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Gaspa anashikilwa na
jeshi la polisi kwa kujiusisha na suala la uganga.
“Sasa nitazunguka nyumba kwa nyumba kwa
ajili ya kusaka waganga wa kinyeji ambao ni wacoichezi wenda nyie ndiyo
munachoma kwa ajili ya kupata wateja na wewe kijana lazima baada ya mkutano huu
niende na wewe kwa ajili ya kuwataja wenzako” alisema Okinda.
Hata hivyo katika mkuatano huo
imeweza kuendeshwa changizo kwa ajili ya wahanga wa matukio hayo ambapo
zimepatikana zaidi ya shilingi laki mbili.
……Mwisho…
|