SERIKALI KUFUTA UJINGA IFIKAPO MWAKA 2030.
|
wadau
mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
|
|
Wanafunzi
wakishiriki maadhimisho hayo.
|
|
Wadau
wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
|
|
Mkutano
ukiendelea.
|
|
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi ya Mbaruku kutoka wilayani Bagamoyo wakiigiza Igizo la Almas
na Jitu kwenye maadhimisho hayo.
|
|
Wanafunzi
wakiwa makini kusikiliza mada.
|
| Wanafunzi kutoka kituo cha kujisomea cha Early Lead Club wakiwa kwenye maadhimisho hayo. |
|
Wadau
na raia wakigeni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
|
|
Ofisa wa
Room to Read kutoka Mikocheni, Veronica Mahenge (kulia), akitoa zawadi ya
vitabu kwa wanafunzi waliosoma vizuri vitabu mbalimbali kwenye maadhimisho
hayo.
|
OFISA Elimu Mkoa wa Dar es Salaam,
Raymond Mapunda kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawe, amesema
serikali itashirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhakikisha
kuwa hadi ifikapo mwaka 2030 wawe wamefuta ujinga nchini.
Mapunda ameyasema hayo jijini Dar es
Salaam jana wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu
kwenye hema yanayoadhimishwa duniani kote.
Alisema moja ya shabaha iliyopo
kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kila mtoto nchini
anapata elimu bure kuanzia darasa la kwaza hadi kidato cha nne.
"Nafahamu shirika lenu la Room
to Read limekuwa likitumia mbinu mbalimbali katika kuendeleza elimu bora kwa
kuweza kujenga maabara katika shule zetu, kutoa vitabu na mambo mbalimballi
katika kupambana na elimu," alisema.
Alisema takwimu za kitaifa za sensa
ya makazi na watu katika mwaka 2012 zinaoonesha kuwa asilimia 22 ya
watanzania hawezi kusoma na kuandika kwa ufasa, 81.7 ni wenye ya msingi 14.4
ndio wenye elimu ya sekondari na asiimia 2.3 elimu ya chuo.
Alisema kiwango hicho kidogo
kinasababisha watoto kutokuwa na msingi imara katika kipindi cha mwazoanapoanza
shule.
"Kwa mfumo unaofanywa na Room
to Read katika kuhakisha wanafunzi wanajua kusomma na kuandika afikapo darasa
la tatu ni wazi kuwa serikali tunapaswa kujifunza ili kuhakisha hadi ifikapo
2030 tunakuwa tumefanikiwa kufuta ujinga," alisema Mapunda.
Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya
maadhimisho hayo inayosema 'Kuandika yaliyoita, Kusoma yajayo' itumike
kutafakari kufuta ujinga.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya
Room to Read, Peter Mwakabwale alisema siku ya usomaji duniani ni siku muhimu
kwa wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi wenyewe, wazazi, walimu, mashirika yasio
ya kiserikali na serikali.
Alisema siku hiyo huadhimishwa kila
mwaka ifakapo Sepemba 9, ikiwa ni kutimiza azimio la Tehrani lilipitishwa
mwaka 1965 ambapo kwa mwaka huu wanaadhimisha miaka 50 tangu kuazshwa kwake
mwaka 1966.
"Kutokana na kuwepo kwa mitiani
ya Taifa ya darasa la saba, sisi Room to Read na washiriki wezetu tuliona
ni vyema kuadhimisha siku hio leo ili kupisha tukio muhimu la wadau wetu,"
alisema.
Mwakabwale alisema takwimu za
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) za mwaka
2015 zinaonesha hali ya usomaji duniani katika nchi saba Jumuia ya Afrika
Mashariki (EAC), Tanzania ni ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha watazania
wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kwa asilimia 80.3.
Alisema nchi ya Burundi inaongoza
katika nchi za ukanda huo kwa asilimia 85.6 ya wananchi wake wanajua
kusoma na kuandika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na nchi nyingine.
Maadhimisho hayo yalinogeshwa na
Taasisi ya Room to Read kwa kufanya maonesho ya vitabu na wanafunzi kutoka
maeneo mbalimbali kupata fursa ya kusoma vitabu na kuulizwa maswali pamoja na
kupata zawadi za vitabu.
KWA HISANI YA BINAG BLOG