MBUNGE COSATO CHUMI AANZA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI.
![]() |
|
Bw
Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends
International akimsikiliza kwa makini Mhandisi wa Maji wa Mji wa Mafinga mkoani
Iringa, Eng Eradius.
|
![]() |
|
Pichani
baadhi ya wanafunzi na waalimu wa shule ya Msingi Makalala wakiwa katika picha
ya pamoja na Mrs Lee na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi.
|
MBUNGE
wa jimbo Mafinga mjini Cosato Chumi ameendeleza juhudi zake za kuwatafutia
maendeleo wananchi wa jimbo lake kwa kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi za
kiserikali na zisizo za kiserikali za nje ya nchi ya Tanzania pamoja na taasisi
za ndani.
Hivi
karibu balozi wa korea nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya
Kutoka Korea ya World
share
alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea changamoto za jimbo
hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya changamoto hizo na
walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.
Baada
ya balozi huyo kurudi jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya
Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la
mafinga mjini na kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo
ambazo alikuwa amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.
Aidha
mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun
Lee alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na
kuzifanyia tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua
kwa kuwa ameshazifanyia utafiti.
“Leo
nimetembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya
Sekondari Luganga na nimejionea shida ya upatikanaji wa
maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa
hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun
Lee.
Bw
Donsun Lee alimpongeza
mbunge
wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za kuwashawishi
kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto ambazo wanaweza
kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.
Katika
ziara hiyo Bw Lee na timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe,
Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga.
Aidha
baada ya tafiti hizo, Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya
Serving Friends International huko Seoul, Korea.
Nia
ya kufanya tafiti hizo ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga
kwa sababu ndo utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani
Singida
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa
NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa
kufanikisha kufanya tafiti ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa
wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na
taasisi hiyo.
Chumi
ameongeza kuwa haya ni matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea
jimbo la Mafinga Mwezi mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.
Lakini
mbunge Chumi amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma
na kuunganisha na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi
inayotakiwa.
“Unakuta
mbunge nahangaika kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini
ukienda vijiweni unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga
soga zisizo na malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la
mafinga mjini litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi


