Benki ya NMB yaendelea kutoa elimu kupitia mkutano mkuu wa ALAT mjini Musoma
| AFISA MKAGUZI MKUU WA NDANI NMB AUGUSTINO MBOGELLA AKIONGEA NA WAJUMBE KATIKA MKUTANO WA ALAT KIPINDI AKITOA MADA. |
| BAADHI YA WATUMISHI WA NMB WAKISILILIZA KATIKA MKUTANO HUO. |
| WAKIHUDUMIA WATEJA |
| PICHA YA PAMOJA WAKIWA NA WAZIRI GEORGE SIMBA CHAWENE |
BENKI ya NMB imeendelea kutoa elimu
kwa viongozi wa halimashauri,manispaa,majiji na wananchi wa kada mbalimbali juu
ya huduma za kibenki ambazo wamekuwa wakizitoa kupitia mkutano mkuu wa 32 wa
Jumuiya ya Tawala na Serikali za Mitaa(ALAT) unaofanyika kitaifa mjini Musoma
mkoani Mara ambapo wajumbe zaidi ya 500 wanahudhuria mkutano huo.
Kupitia mkutano huo NMB imeelezea jinsi ilivyounganisha mfumo wake wa kibenki na mfumo wa serikali za mitaa (LGRCIS) kufanikisha ukusanyaji mapato ya kwa wakati na bila kupotea na kuandaa vituo vya makusanyo ya fedha kusaidia serikali katika makusano.Akitoa mada kwenye mkutano huo ulioingia siku ya 2 hii leo,Afisa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa (NMB)Augustino Mbogella,amesema licha ya kusaidia serikali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato,benki hiyo pia imesaidia miradi ya maendeleo ya jamii ikilenga zaidi katika utoaji wa misaada katika sekta ya elimu na afya.

Amesema mwaka 2015 pekee zaidi ya
shule 140 za msingi na sekondari zilipata zaidi ya madawati 7,000 kwa Tanzania
nzima katika mpango wa kuendelea kutatua tatizo la madawati mpaka kufikia
septemba 2016 tayari wametumia zaidi ya milioni 900.
Mbogella amesema kwa upande wa afya wametoa vifaa mbalimbali kwenye hospitali 50 za serikali pamoja na vituo vya afya ambapo kiasi cha fedha takribani shilingi milioni 200 zilitumika.
Mbogella amesema kwa upande wa afya wametoa vifaa mbalimbali kwenye hospitali 50 za serikali pamoja na vituo vya afya ambapo kiasi cha fedha takribani shilingi milioni 200 zilitumika.
Viongozi na wananchi wameombwa
kutembelea banda la NMB ili kuweza kupata elimu zaidi ikiwepo pia suala la
ufunguaji wa akaunti mbambali kwenye benki hiyo ambazo zina manufaa makubwa.