|
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AKINYANYUA NDOO YA MAJI BAADA YA KUZINDUA RASMI MRADI HUO WA MAJI KIJIJI CHA KISUMWA WILAYANI RORYA MKOANI MARA
Wanawake
wilayani Rorya mkoani Mara wamesema kuwa wataendelea kuzaa vyema baada ya
kuondokana na hadha ya huduma ya maji suala ambalo lilikuwa ninawalazimu
kuamuka majira ya ya usiku na kuwaacha waume zao wakiwa wamelala huku
wakitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata maji
Hayo
yamebainishwa hivi karibuni kipindi Mwenge wa uhuru ulipokuwa ukizindua mradi
wa maji katika kijiji cha kisumwa wilayani
Rorya mkoani Mara ambapo mradi huo wa maji umegalimu shilingi millioni 633 huku
ukitarajia kuhudumia idadi ya watu 2618 sawa na kaya 524
Wakina mama
ao walidai kuwa kitendo cha hadha ya maji katika kijiji cha Kisumwa kimewakumba
kwa muda mrefu suala ambalo lilikuwa linapelekea wanawake kuamka usiku na kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta
huduma ya maji na kushindwa kulala na aume zao mpka asbuhi.
“Maji hapa
yalikuwa ni kero kubwa hatulali na wanaume zetu tunatembea umbali mrefu wakati
mwingine wengine wanatishiwa kubakwa kwani ni usiku wa manane hautfurahia ndoa
zet sasa tutazaa kwa wingi kwa sababu maji yametufikia karibu” walisema kina
mama hao.
Emmanuel
Masanja ni Mwandisi wa maji Wilayani Rorya Mkoani mara alisema kuwa mradi huo
ni Miongoni mwa miradi mikubwa inayotelezwa chini ya mfumo wa Tekeleza sasa kwa
matokeo makubwa ambapo alisem akuwa unatariajia kuhudumia watu2618 sawa na kaya
524.
Kwa upande
wake kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa George Jackson amewataka wanachi wilayani
rorya mkoani mara kuendelea kulinda miundombinu pamoja na vyanzo vya maji nakuondokana
na suala la kuharibu miundombinu kwa ni suala hilolinachangia kurudisha
naendeleo nyuma.
Pia
amewataka wakulima wa kilimo cha umwagiliaji Chereche kuendelea kulinda vyanzo
vya maji na kuendelea na umoja wao katika kudumisha kilimo hicho.
Hata hivyo
kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa amewataka vijana kuondokana na suala la
kuchagua kazi huku wakibagua kilimo bali wajikite katika suala zima la kilimo
huku wazazi na walezi Mkoani Mara wakitoa ushirikiano mkubwa kwa walimu wa
shule za msingi na sekondari ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao.
Mwaka huu
kauli mbiu ya mwenge wa uhuru Vijana ni
Nguvu kazi ya Taifa washirikishwe na kuwezeshwa
|