MADIWANI TARIME HOSPITALI ZA BINAFSI ZINAZOTOA HUDUMA YA DAMU SERIKALI INGILIA KATI.



Madiwani halmashauri ya wilaya yaTarime mkoani mara wamesema kuwa ili
kuokoa maisha ya watanzania hakuna haja ya hospitali za watu binafsi kutoa
huduma ya damu kwa wagonjwa.


Hayo yamebainishwa na diwani wa viti maalumu chadema philomena Tontola
kipindi akichangia katika baraza la madiwani lilofanyika hivi karibuni
katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime.


Philomena amesema kuwa suala la kuongezwa damu holela linaweza kuwa chanzo
kikubwa cha uchochezi wa maambukizi ya virus vya Ukimwi hivyo serikali
haina budi kuingilia kati kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzani
Alitolea mfano baadgi ya hospitali zilizopo nyamongo zinatoa huduma ya damu wananchi wako hatarini kwani damu hizo siyo salama kwa afya ya wananchi hao.


Hata hivyo  diwani huyo amesema kuwa taratibu za upatikanaji damu zinafaamika
hata hospitali kubwa upata damu kutoka banki kuu ya damu baada ya
kuhakikiwa ubora wake sasa hospital binafsi zinazoroa huduma ya damu hazitazidi
kuhatarisha maisha ya watanzania.


Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime Moses Misiwa anemwagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya TarimeApoo Tindwa kushirikiana na
mganga mkuu na wataalamu wa Afya ili kubaini hospitali zinazokiuka taratibu
na kuchukuliwa hatua kali kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania



Powered by Blogger.