MADIWANI HALMASHAURI YA TARIME WAJITOKEZA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI.
| DIWANI WA KATA YA BINAGI AKIPIMA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI HII LEO |
| DIWANI WA KATA YA NYARERO MHABASI AKIPEWA KARATASI YENYE NAMBA KWA AJILI YA KUPIMA |
| MMOJA WA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME AKIPIMA HII LEO |
| DIWANI WA KATA YA KEMAMBO AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA TARIME RASHID BUGOMBA AKIPIMA |
Ili kuweza kuhamasisha wananchi Wilayani Tarime mkoani Mara
waweze kujitokeza kwa lengo la kupima maabukizi ya Virusi vya Ukimwi ili kujua
Afya zao na kuanza kutumia dawa za ARV, Madiwani katika Halmashari ya Wilaya ya
Tarime mkoani Mara wamejikeza kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi kabla ya
kuanza baraza la madiwani la kawaida kwa lengo la kujua Afya zao ili kuwa mabalozi
wazuri katika vijiji na kata kwa lengo la uahamasisha wananchi kujitokeza
kupima.
Zoezi hilo limeendelea hii leo kabla ya kuanza kikao cha
baraza la madiwani ambapo madiwani hao wamejikokeza kwa wingi kwa lengo la
kupima ili kujua afya zao ambapo katika kikao kilichoisha madiwani hao waliweza
kuazimia kupima wote wakiwemo watumishi wa Halmashauri ili kuweza kujua Afya
zao.
John Mhabas ni diwani kata ya Nyarero ambaye pia alileta
hoja hiyo ya madiwani kujua Afya zao katika balaza la madiwani lililopita alisema
kuwa suala zima la kupima ni jukumu lao kama viongozi wa wananchi ili kuweza
ili kuweza kuwa mabalaozi wazuri katika sula zima la kuhamaisha upimaji wa
maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Aidha Mhabas aliongeza kuwa endapo diwani yeyote atakutwa
ameambukizwa Virusi vya ukimwi ataweza kuunda kikundi na kuweza kuhamasisa
wagonjwa wengine ili kuendelea kutumia dawa za kulefusha maisha ili kuendelea
kuishi.
Moses Yomamami
nimwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime amesema kuwa maendeleo yeyote
yanayofanywa na kiongozi lazima aweze kuwa na afya iliyonjema hivyo suala la
afya limewalazima kupima ili kuweza kujua afya baada ya kuazimia japokuwa
sheria ya kupima virusi vya ukimw ni kupima ni hiari ya mtu na siyo
kulazimishwa japokuwa wao kama madiwani waleweza kuazimia na kuweza kutimizza
zoezi zima.
Naye Veronica Sando diwani wa viti maalumu CHADEMA aliongeza
kuwa suala zim ala kupima limemufuraisha kwa madiwani wenzake kujitokeza kupima
huku akisema ugonjwa Ukimwi ni kama ugonjwa Mwingine hivyo suala zima la kupima
kwa madiwani hilo ni chachu kubwa kwani madiwani wakianza kuhamasisha wananchi
bila kupima zoezi litakuwa gumu.
| DIWANI WA VITI MAALUMU CHADEMA AKIPEWA MAELEKEZO NA KATIBU WA AFYA WILAYA YA TARIME NEEMA ALPHONCE |