ACACIA WAKABIDHI BILLIONI 1.3 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME USHURU WA HUDUMA.
![]() |
| MENEJA MSADIZI ACACIA JOHN CONNELL AKIKABIDHI MFANO WA HUNDI YA BILLIONI 1.3 KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME MOSE YOMAMI WA KWANZA KULIA NI AFISA MAHUSIANO ZAKAYO KAREBO |
Mgodi wa dhahabu wa Acacia uliopo nyamongo wilayani
Tarime mkoani mara umekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 Fedha za mrahaba kama ushuru wa huduma (service Levy) kwa serikali katika
halmashauri hiyo kwa ajili ya fedha hizo kwenda kufanya maendeleo ya wananchi ikiwemo huduma ya Afya Elimu Maji na
barabara.
Akipokea hundi hiyo mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Tarime mkoani mara Moses
Yomami amebainisha kuwa fedha hizo zitaelekezwa mojakwa moja katika shughuli za
wananchi ikiwemo kufanya maendeleo ikiwa ni pamoja na mgodi huo kuongeza fedha
za mrahaba huo baada ya halmashauri kuhoji jumla ya fedha zinazozalishwa na
mgodi huo kwa muda wanotoa fedha hizo .
Glorious Luoga ni mkuu wa wilaya ya Tarime
ameihakikishia halmashauri hiyo kusimamia na kuhakikisha fedha hizo zinafanya
kazi kwa uhakikia huku akitoa kalipio kali kwa wataaakao hujumu fedha hizo na
kusema kuwa wataweza kufikishwa mahakamani pale watakapobainika ili kurudisha
fedha za serikali.
Kwa upande wake kaimu meneja wa mgodi wa Acacia
uliopo nyamongoWilayani Tarime Mkoani mara John Connell amesema kuwa fedha hizo
za mrahaba hazina budi kulekezwa kwa wananchi ili waweze kujua mgodi huo unatoa
fedha hizo ikiwa ni pamoja na kutekeza miradi ya wanachi ili kujivunia uwepo wa
mgodi huo.

