Binti mmoja
Mkazi wa kijiji cha Kemakorere Kata Nyarero Wilani Tarime Mkoani mara Mwenye
umri wa miaka 16 Maria Mahiya amezidi kuiomba Serikali kwa kushirikiana na
mshirika mbalimbali ikiwemo jamii inayozunguka watu wenye ulemavu wa Ngozi
albino kutoa msaada ili kuweza kutibiwa saratani ya sikio ambayo imedumu kwa
muda mrefu bila kupona jambo ambalo linamusababishia maumivu makali.
Maria
alisema kuwa alianza kupata upele katika sikio hilo ambapo baba yake mzazi
alifanya jitiahada za kumpeleka Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya
Wilaya hadi mkoa lakini kadili alivyozidi kupata matibabu hali yake ilizidi
kubadilika na kulazimika kupelekwa Hospitali ya Ocean Road lakini bado hali
yake ni mbayo hivyo ameiomba serikali kumpa msaada ili kupata matibabu kwa
lengo la kuokoa maisha yake.
“Mimi kwa
kweli hali yangu ni mbaya sana naomba rais wetu akasikie kilio change na
kunipeleka Nje ya Nchi ili nipate matibabu kwa ajili ya kunusuru maisha yangu
jamani” alisema Maria huku akilia kwa uchungu.
Mahiya
Matiko 43 ni baba mzazi mwenye watoto11 huku watoto wawili wakiwa ni walemavu
wa Ngozi albino ambapo mke wake kwa sasa ni mwaka wa pili amefariki dunia hivyo
family yake inamutegemea amesema kuwa kwa sasa ameisha uza malizake zaidi ya
millioni moja ili kutibu mtoto wake ambaye anasumbuliwa na saratani ya sikio
yenye uvimbe sikioni hivyo amezidi kutoa kilio kwa serikali na mashirika ili
kumusaidia mtoto huyo.
“Jamani huyo
mdogo wake alinusurika hivi karibuni kuibiwa na watu wasiojulikana
sasanikampeleka kituo cha kutunza watoto wenye ualbinodada yake amekaa Dar es
salaam takribani miezi saba ocean road hajapona amerudi kila siku ni lazima
kuosha kidodo sina hata mia sasa mimi bora mungu amuchukue sina jinsi serikali
inisaidi sasana watu wenye huruma kupitia namba0766128337” alisema Mahiya.
Eliza James
Ni katibu wa Chama cha watu wenye Ualbino Wilayani Tarime Mkoani Mara (TAS)
watu wenye ulabino wamesahulika huku jamii imekuwa ikiwatenga na kusema kuwa
adui wao mkubwa ni jua sasa serikali haina budi kuwasaidia ili waweze
kujikwamua kiuchumi.
Sisi mbali
na mauaji lakini hayo serikali imekomalia lakini adui wetu ni jua na wengi
wenzetu hawajaenda shuleni na hatuwezi kufanya kazi za juani serikali isikie
kilio chetu hususuani cha marai mwenzetu anaumia sana nimekwenda mwanza
kumpokea akitoka kwenye ,matibabu hadi kufika Tarime nimembeba anamaumivu
makali alisema Eliza.
PICHA NA KARORY JACOB
|