WAHANGA WA UKATILI WA KIJINSIA TARIME CDF YAWAPA MAFUNZO YA UJASILIAMALI.
AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYANI TARIME MKOANI MARA VICTOR KABUJE KATIKATI AKIONESHWA BAADHI YA BIDHAA ZILIZOTENGENEZWA NA WASICHANA HAO KULIA NI MENEJA SIDO MKOA WA MARA FRIDA MUNGULU. |
Wilayanni
Tarime Mkoani Zaidi ya wasichana 50 wakiwemo ambao wamekumbwa na vitendo vya
ukatili wa kijinsia ukewemo ukeketaji, Ndoa za Utotoni, Ugumu wa Maisha na
kupelekea kuacha masomo, Wasichana wanaishi katika maisha magumu pamoja na mimba za utotoni wamepata mafunzo ya
ujasiliamali ukiwemo utengenezaji wa Sabuni pamoja na Batiki ili kuwezakujikimu
na kujiinua kiuchumi kwa lengo la kuondokana na utegemezi huku wakifundishwa
kwa lengo la kuwa mabalozi vijijini na kusamabza Elimu hiyo.
Mafunzo hayo
yametolewa hivi karibuni katika ukumbi wa Roma Springi Hotel Halmashauri ya Mji
wa TAarime Mkoani Mara takribani siku
Nne ambapo washiriki wa mafunzo hayo wamezidi kuiomba serikali kuwaunga mkono
kwa kuwapa mikopo yenye riba kidogo ili kuweza kununu mali ghafi kwa ajili ya
kutengeneza bidhaa hizo.
Aines Chacha
kutoka kata ya Manga alisem akuwa kabla ya kupata mafunzo hayo baada ya kukosa
ada ya sule aliweza kuacha shule na kuendelea na shughuli za kilimo kwa
kushirikiana na wazazi hivyo baada ya kupata mafunzo hayo itamusaidia katika
kujikwamua kiuchumi huku akiwasihi wenzake kuwa walimu ili kila msicha ambaye
amekumbwa na janga aweze kujikwamua kiuchumi.
Kambibi
Kamugisha kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali Jukwaa la utu wa Mtoto CDF
Amesema kuwa mafunzo hayo yameshirkisha watoto wa kike kuanzia miaka 18 mpaka
24 ambap baadhi yao ni wahanga wa ukatili wa kijinsia ukiwemo Ukeketaji na Ndoa
za Utotoni hivyo kama shirika limetambua hilo mabli na kuwapa Elimu juu ya
kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia wameamua kuwapa Elimu ya Ujasiliamali
ili waweze kujinuka kiuchumi.
Aidha
Kamugisha aliongeza kuwa Shirika hilo pia Kwa kushirikiana na Shirika la
Forward lililpo UK Chini ya Ufadhili wa shirika la COMIC RELIEF,SIGRID RAUSINGbaada
ya wasichana hao kuopata mafunzo hayo wataweza kuunda makundi ili kuweza kupewa
mikopo isiyokuwa na riba na yenye mashariti nafuu ili waweze kurejesha nakuweza
kukopesha vikundi vingine.
“Mafunzo
haya yameshirikisha kata Tano ikiwemo kata ya Manga, Matongo,Susuni,Mwema na
Nkende na zaidi ya wasicha 50 wamepata mafunzo na tulikuwa tumelenga wasicha 60
na muradi huu ni watakribani miaka mitatu ambapo tumelenga kukomboa mtoto wa
kike wilayani Tarime” alisema Kamugisha.
Kwa upande
wake Meneja wa SIDO Mkoa wa Mara Frida Mungulu alisema kuwa sasa ni matumaini
kwa wasichana hao kuenda kufanya kazi kwa ufanisi huku viwanda vya batiti na
sabuni vikizidi kuongezeka nakuwaomba kutimia vyema mikopo watakayopewa na CDF
ili badae watakaporejesha vyema waeze kukopa katika Taasisi nyingine za kifedha
kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Akifunga
Mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya jamii Victor Kabuje amedai kuwa kufundishwa kwa
wasicha hao itakuwa chachu ya kusukuma maendeleo katika jamii huku akiwataka
wasichana hao kwenda katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kupitia Ofisi za
Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kusajili vikundi vyao ili serikali iweze kuwapa
mikopo.
“Tayari
mmepata Fursa ana sisi kama serikali tunasukuru shirika la CDF Kwa sababu
wamefanya kazi ambayo ingefanywa na ofisi yangu lakini kutoka na changamoto za
rasilimali fedha hebu tumieni vyema fursa hiyo na ofisi zangu ziko wazi njoo
niwape vyeti vya usajili kupitia makundi yenu ili na sisi serikali tuwape
mikopo na nyie muwe mabalozi wetu katika kusambaza Elimu hiyo” alisema Kabuje.
Aidha Kabuje
ameongezakuwa kuwa akina mama wilayani Tarime hawana budi kutumia fursa iliyopo
baina ya mpaka wa Tanzania na kenya huku akilaani vikali vitendo vya ukatili wa
kijinsia ambavyo vinafanywa na jamii ukiwemo Ukeketaji na Vipigo kwa wanawake.