WAGANGA TIBA ASILI WATAKIWA KUJISAJILI.
PICHA YA MWAKILISHI WA CHAMA CHA TIBA ASILI TANZANIA MKOANI MARA JACOB MATIKO AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI. |
wanachama wa
chama cha tiba asili tanzania chawatiata mkoani mara wametakiwa kujikita kwenye
usajili wa baraza la tiba asili na tiba mbadala unao simamiwa na wizara ya afya
ili kuepukana na utitiri wa vyeti ambavyo wanapewa kwa kuaminishwa kuwa ndivyo sahihi kwao.
Hayo
yamebainishwa na na mwakilishi wa chama
hicho mkoani mara Jacob Matiko,akiwa
ofisini kwake mjini musoma, baada yakupata malalamiko kutoka kwa wanachama hao
kuwa ,kuna vyeti ambavyo waganga wa tiba asili wanapewa na kulipishwa zaidi ya
shilingi elfu 30 kwa kila cheti jambo ambalo linadidimiza usajili wa baraza la
tiba asili na tiba mbadala unao wataka waganga kusajili kupitia baraza hilo kwa
kujaza fomu namba moja,kwa mujibu wa sheria no 23 ya mwaka 2002.
Aidha Matiko
ameongeza kuwa vyeti hivyo ambavyo vimekuwa vikitolewa na aliyekuwa mwenyekiti
wa zamani wa chombo cha shirikisho la vyama vya tiba asili tanzania bwana
Abdulrahaman Musa lutenga siyo kamilifu kwani kwa mujibu wa katiba ya chombo
hicho,hakuna sehemu inayosema shirikisho linatakiwa kutoa vyeti kwa mganga
mmoja mmoja na badala yake linatakiwa
kutoa vyeti hivyo vya heshima kwa vyama washirika,taasisi,mashirika pamoja na
asasi mbali mbali.
Hata hivyo
Jacob ameongeza kuwa hatakubali
wanachama wake kulaghaiwa na chombo hicho kwa kuwapa waganga vyeti hivyo,na
badala yake amehimiza wanachama wake na
waganga wa tiba asili kwa ujumla kusajiliwa
ndani ya baraza la tiba asili nchini ili kuepusha mikanganyiko hiyo.
Sambamba na
hayo imesemekana kuwa endapo viongozi hao wa zamani wa shirikisho wataendelea
kutoa vyeti vya shirikisho kwa mganga mmoja mmoja, wizara ya afya isitarajie
kuona kasi ya usajili kwa waganga wa
tiba asili kwani wanapo pata vyeti hivyo vya shirikisho wana amini kuwa tayari
wamesajiliwa.
Akielezea
kuwepo kwa ziara ya bwana lutenga mkoani mara kama mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya tiba
asili nchini,bwana matiko amesema si kitendo cha busara kwani bado upo mgogoro
mkubwa wa vyama vya tiba asili nchi na mwenyekiti huyo na inatakiwa kurudi na
kukaa chini na viongozi wa vyama vya tiba asili ili kuondoa tofauti zao ndani
ya chombo hicho,ili waweze kulisogeza mbele hili gurudumu la tiba asili nchini.
Hata hivyo
Matiko amezidi kukemea na kulaani vikali
kitendo cha Bwana Lutenga kumuita katibu mkuu wa chama cha chawatiata
bwana mittamu magombe kwamba ni tapeli na kurusha maneno hayo katika mitandao
ya kijamii,jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria za mitandao, Aidha bwana
matiko amemtaka bwana lutenga kutoa ushahidi kuhusu utapeli wa katibu mkuu wa
chama hicho cha chawatiata hapa nchini.
Akielezea
barua aliyo peleka kwa viongozi wa serikali inayo elezea kuhusu kuto kuutambua
ujio wa bwana lutenga mkoani mara kama mwenyekiti wa shirikisho taifa, bwana
matiko amesema ni kweli kwani wao kama
viongozi wa vyama hawakupata taarifa zozote kuhusu ujio huo, napia kwa sasa
chama chao hakimtambui bwana lutenga kama mwenyekiti wa shirikisho hilo la
vyama vya tiba asili nchini hadi pale watakapo maliza tofauti zao na vyama
washirika wa chombo hicho cha shirikisho nchini.
Akimshukuru
katibu mkuu wizara ya afya dr mpoki, bwana matiko amesema kuwa,baada ya katibu mkuu wizara ya afya kupata taarifa
hizo za waganga kupewa vyeti vya shirikisho kinyume na utaratibu,katibu mkuu
alitoa ufafanuzi kuwa waganga wanatakiwa kujisajili ndani ya baraza la tiba
asili kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 2002,lakini pia amesikitishwa na
bwana lutenga kwa kile alichokiita ni ukosefu wa busara kutoka kwa bwana
lutenga, kwani kuna mgogoro bado unaendelea ndani ya chombo hicho na kushauri
asubiri kwanza mgogoro huo upatiwe uvumbuzi na ndipo aende kwa waganga
kujitangaza kama mwenyekiti wa shirikisho hilo nchini endapo atapewa ridhaa
hiyo na vyama washirika.
Matiko amewataka wanachama wa chama hicho kuwa
na subra kipindi hiki ambacho vyama bado vinaendelea kulipatia uvumbuzi swala
hili la shirikisho la vyama vya tiba asili nchini, nakueleza kuwa kwa sasa
katika mkoa wa mara haumtambui kiongozi yeyote anaye jiita ni kiongozi wa
shirikisho la vyama vya tiba asili kuanzia ngazi ya wilaya na mkoa hadi pale
yatakapo tolewa maelekezo kutoka makao makuu kuhusu namna ya kuwapata viongozi
hao wa shiurikisho, na ameeleza kuwa yeye bado ni mwakili wa chama hicho mkoani
mara, hadi pale makao makuu ya chama hicho yatakapo tengua uwakilishi wake
mkoani mara,