JAMII YATAKIWA KUTUNZA NYARAKA
PICHA YAMRATIBU WA MRADI WA KUZUIA UKATILI WA KIJINSI KATIKA WILAYA YA BUNDA NA TARIME MKOANI MARA ASIYA MUYA AKIFAFANUA JAMBO KWA WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO. |
JAMII YATAKIWA KUTUNZA NYARAKA.
Jamii
imehaswa kujenga tabia za kutunza nyaraka mbalimbali ikiwemo utunzaji wa vyeti
vya ndoa kwa lengo la kusaidia mashirika mbalimbali ambayo yamekuwa yakitetetea
haki za binadamu ili pale changamoto zinapojitokeza katika ndoa ikiwemo kudai
mirathi kwa wanandoa hao na shauri hilo kufikishwa mahakamani ili kuwepo
ushaidi wa kutosha kwa lengo la kupata hakizao za msingi na masirika hayo
yaweza kufanya kazi kwa ufanisi.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Kivulini
lilopo jijini Mwanza Bw Yassin Ally wakati wa kutoa mafunzo kwa wanaharakati wa
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo wanaharakati125 kutoka baadhi ya
kata zilizomo ndani ya wilaya ya Tarime wanatarajia kupata mafunzo hayo
takribani wiki moja huku kata za
kibasuka ,Binagi, Muriba, Ganyang’e,na Bumera tayari wanaendelea na mafunzo
takribani wiki moja pia mkurugenzi huyo amewaomba watanzania wote kujenga tabia
ya kutunza nyaraka mbalimbali zikiwemo hati za nyumba pamoja na Mashamba.
Ally alisema
kuwa kutokana na changamoto za jamii wakiwemo wanandoa kushindwa kutunza
nyaraka vikiwemo vyeti vya Ndoa, Vyeti vya Watoto, Hati za Nyumba na Mashamba
inapotokea changamoto pale mmoja kati ya wanando kudai haki zake aidha baada ya
kupeana taraka au mmoja kufariki mashirika hayo upata Changamoto pale mahakama
inapodai ushaidi.
“Hivyo
kunawajibu mkubwa watanzania wote kutunza nyaraka hizo ili kutusaidia sisi pale
tunaposimama mahakamani kuwatetea ili kuwa na usaidi wa kutosha ili kushinda
kesi na jamii huska kupata haki zao”alisema Ally.
Hata hivyo
Ally aliongeza kuwa jamii pia haina budi kuondokana na tabia ya kuwapa watoto
majina ambayo siyo ya wazazi wao kwani
kitendo hcho kinawanyima watoto hao haki zao za msingi pale baba mzazi
anapojitokeza kudai mtoto wake na kukuta cheti cha mtoto kimeandikwa jina la mjomba
wa mtoto huyo.
“Mfano wale
watoto wanazalishwa na baba wa nje ya
ndoa upewa majina ya wajomba zao na pale inapofikia hatua hati ya nyumba
imeandikwa jina la mtoto huyo uleta changamoto kujua nani mwenye nyumba hiyo”
alisema Ally.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara Ndoa
nyingi ni za kimila ambapo zinapelekea baadhi ya Nyaraka kuhusu ndoa hizo
utunzwa na wazee wakwe badala ya wanandoa kati ya Mme na Mke ambapo uleta
changamoto pale mjane anapotaka kudaia miradhi na anapofika mahakamani ukosa
ushaidi hivyo amewaomba wanandoa hao na jamii kwa ujumla kuwa na utaratibu wa
kutunza nyaraka.
“Unakuta
wanandoa wawili baina ya mwanamke na mwanaume wanapofunga ndoa nyaraka ubaki
kwa baba mkwe wa binti na kijana na wanandoa hao hawana nyaraka ikitokea
mtafaruko kwa mjane kudai haki zake na shauri kufika mahakamni inakuwa changamoto
kubwa hivyo kuna haja kubwa wanandoa hao kutoa kopi ya nyaraka hizo nao
kuzitunza” alisema Yassin.
Daniel
Nyiraha mkazi wa kijijicha Magoma kata ya
Binagi alisema kuwa baada ya kupata
mafunzo hayo tayari wamegundua dosari huku wakihaidi kwenda kufikisha Elimu
hiyo kwa jamii ili kuweza kuondokana na dhana potofu pamoja na vitendo vya
ukatili pamoja na kuondokana na imani ambazo zinakinzana na sheria huku
wakitaja changamoto wanazokumbanazo katika utendaji kazi wao.
“Sasa sisi
kama wanaharakati ambao tayari tumepata mafunzo haya ni wajibu wetu sasa
kufikisha Elimu hii kwa jamii ili kuondokana na dhana potofu ambazo zinakinzana
na sheria” aliseam Daniel.
Naye Martha
Simion Kutoka kata ya Muriba Wilayani Tarime alisema kuwa katika kutoa Elimu
kwa jamii ili kuondokana na ukatili wa kijinsia baadhi ya wanajamii hawako
tayari kupokea Elimu hiyo huku wakidai kuwa wanaharakati hao wanapokuja kupata
Elimu upewa fedha.
Lakini sisi
kwa sababu tumejitolea ili kusaidia jamii yetu hatutakata tama ili kusaidia
wananchi ili kuondokana na vitendo vya ukatili vikiwemo vipigo kwa akina mama
pamoja na kupata hakizao ikiwemo mirathi kwa wajane alisema Martha.
PICHA YA AFISA MAENDELEO YA JAMII WILYAYANI TARIME MKOANI MARA SIWEMO OTIENO AKIELEZEA JAMBO KWA WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO. |
MTENDAJI WA KATA YA KIBASUKA WILAYANI TARIME MKOANI MARA MWITA MUTATIRO AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WANASEMINA HAO. |
MRATIBU WA MRADI AKISISITIZA JAMBO. |
MMOJA WA WANASEMINA HAO AKIELEZEA MADA. |
WANASEMINA WAKISIKILIZA SOMO KWA MAKINI. |
MTENDAJI WA KATA YA KIBASUKA MWITA MUTATIRO AKISISTIZA JAMBO KWA WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO. |