WAUGUZI WALILIA STAHIKI ZAO NA SARE ZA KAZI




WAUGUZI WALILIA STAHIKI ZAO NA SARE ZA KAZI

Wakati wauguzi wakiadhimisha siku ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa uuguzi duniani inayoadhimishwa mei 12 ya kila mwaka, katika halmashauri ya mji wa Tarime wauguzi  wameitaka serikali kutatua ukosefu wa sare za kazi na kuboresha mazingira ya utoaji tiba na vifaa tiba.

Aidha  wauguzi hao wameitaka serikali kulipa stakihiki zao kwa wakati ikiwa ni hatua ya kuwafanya waongeze ari ya kuwajibika na kutekeleza majujumu yao kulingana na wito wao.

Akisoma risala wakati wa sherehe hizo zilizofanyikia katika ukumbi wa chuo cha uuguzi Tarime(NTC) katibu wa chama cha wauguzi Tanzania tawi la Tarime Mokami Mirumbe alisema wauguzi wamekuwa wakijinunulia safe za kazi kwa kipindi cha miaka mitatu jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Katika taarifa hiyo alisema kuwa halmashauri ya mji wa Tarime ina jumla ya wauguzi 89, wenye shahada watano, stashahada 13 na cheti 67 ambao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali na kuwakwamisha kutimiza wajibu wao.

Walitumia nafasi hiyo kuitaka serikali kutatua matatizo yanayowakabiri wauguzi ikiwa ni kuongeza idadi ya wauguzi kuendani na wingi wa wagonjwa, ikiboresha mazingira ya kazi na kuwapa wepesi wa kuwahudumia wateja wao kikamilifu.

Aidha walisema kuwa hospitali na vituo vya Afya vinakabiliwa na uhaba wa walinzi hali inayowafanya jamaa wa wagonjwa kulala wodini kuwalinda ndugu zao hali inayofanya siri za kazi kuvuja.

"Ulinzi katika vituo vyetu vya kazi ni wa kutia shaka kwani kumekuwepo na tatizo la ndugu wa waginjwa kuingilia utendaji kazi wetu na kutufanya tushindwe kufanya kazi ipasavyo hasa nyakati za usiku kutokana na kutikuwa na walinzi Wa kutosha" alisema Mirumbe.

Akiongea na wauguzi hao mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Tarime Deusdedith Magoma aliwataka kufanya kazi kulingana na mazingira kwani serikali imejipanga kuyapunguza matatizo yanayokabili sekta hiyo kwa asilimia 60 katika bajeti ya mwaka 2016/2017.

Hata hivyo aliwataka kubadilika katika utendaji kazi yao kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya nne inayoweka mbele uwajibikaji na kuwahudumia wananchi huku akiwatadharisha kuwa makini na kauli za wateja wanaowahudumia.

" Watakuja wauguzi hapa wanafanyakazi, wengine ni wagonjwa watalazwa humu au wanawauguza wagonjwa wao kumbe wako kazini na baada ya kumaliza kazi yao, matokeo yake utajikuta mambo yamekuharibikia na huna mtu wa kukusaidia kuyatatua maana muda umeishakupita" aliwataharisha wauguzi.


Powered by Blogger.