WALIMU WAJIVUNIA KUPATA ELIMU YA KUJIENDELEZA.
PICHA YA MRATIBU WA KITUO CHA WALIMU WILAYANI TARIME MKOANI MARA SOPHIA RANGE AKIONGEA NA CLEO NEWS HII JANA. |
Kumekuwepo
na malalamiko mbalimbali kuhusu ruhusa za waajili hususani wakurugenzi wa
Halmashauri mbalimbali hapa nchi kuwapa walimukatika shule za msingi na
sekondari ruhusa kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo kwa lengo la kuongeza
ufahamu na kuboresha taaluma hapa nchini kwa kuliona hilo sasa walimu shuleza
msingi wameweka mikakati na mbinu
za kuweza kujiendeleza wakiwa kazini kwa
lengo la kupata Elimu ngazi ya Diploma ili kuondokana na elimu ngazi ya daraja la tatu
“A”cheti wengi walionayo.
Akiongea na
jamb oleo mratibu wa kituo cha walimu
Wilayani Tarime mkoani Mara Sophia Range
alisema kuwa kwa sasa wameanza mafunzo
ya walimu kutoaka daraja la tatu A kwenda kwenda kiwango cha Diploma kwa
kushirikiana na na chuo kikuu Maunt meru Tawi la mwanza ambapo walimu
wamejitokezeza kwa wingi ili kuweza kupata Elimu hiyo.
Alisema kuwa
walinza na walimu wachache lakini kadri muda unapoenda walimu wanazidi
kuongezeka ambapo kwa sasa takribani wiki tatu tagu kuanza kwa masomo hayo
alisema kuwa walimu wote ambao hawajapata fursa ya kujiunga hawana budi kujiunga kwa ajili ya kupata
fursa hiyo ambayo imewafikia karibu ili kuweza kuifaidi.
“Walimu
wengine walikuwa wakikumbwa na changamoto ya kutoenda masomoni aidha kwa kukosa
ruhusa kutoka kwa waajili na wengine kipato pamoja na vyuo vya kujiendeleza
kuwa mbali sasa huduma hii inapatika Tarime ktika na pia nashangaa kuona walimu
wa Halmashauri ya mji wa Tarime ambapo wako mjini na huduma hiko karibu lakini
wamejitokeza kidogo takribani walimu wanne na Halmashauri ya wilaya ya Tarime
ni takribani walimu 31 pia wapo walimu wawili kutoka wilaya jirani ya Rorya
wameomba kujiunga kwani mafunzo haya hayaharibu utendaji kazi na masomo haya
uanza ijumaa mpaka jumapili jioni” alisema Mwl Range.
Hivyo basi
katibu huyo amezidi kutoa wito kwa walimu ambao hawajapata fursa ya kujiunga
mwezi April wajiandae kwa mwezi Agosti ili kuakikisha kila mwalimu wakiwemo
walimu wa kike ambao mara nyingi changamoto ya kifamilia imekuwa ikichangia
wasiweze kujiendeleza kutumia fursa hiyo.
Hata hivyo
Mratibu huyo amezitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na upungufu wa
majengo nab ado majengo waliyonayo yanavuja pia mwitikio wa walimu umekuwa mkubwa kwa
maana walimu watakaoingia mwezi Agosti watakosa majengo hivyo ametumia fursa
hiyo kuwaomba wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili Halmashauri ya mji wa Tarime
na Wilaya pamoja na wabunge a majimbo yote mawili kuwaunga mkono ili kutatua
changamoto hiyo ili kuboresha Elimu.
Hata hivyo
Mwalimu Sophia aliongeza kuwa kituo
hicho siyo fursa kwa walimu tu bali anampango wa kuongeza masomo ya
kujiendeleza kwa muda wa miaka miwili ikiwa ni pamoja na kurudia mtihani kwa
vijana wa kidato cha Nne ambao hawakukidhi viwango vya ufaulu na mambo hayo yot
yanahitaji majengo hivyo ni jukumu la wadau wa Elimu kuungana pamoja ili kuweka
changizo kwa lengo la kuwaunga mkono na kufikia malengo.
“Mpango
wangu ni kukiendeleza kituo hiki kutoka ngazi ya walimu na kuhakikisha wanachi
wakiwemo wanaotaka kujiendeleza pamoja na vijana wetu wa kidato cha nne kuweza
kupata masomo ili kubadili Tarime ambayo haikuwa na mtazamo wa Elimu huko nyuma
na hayo yote ni ushirikiano” alisema Mratibu huyo.
Nao baadhi
ya walimu ambao tayari wameisha anza masomo hayo wamedai kuwa jambo hilo
litakuwa mkombozi kwani huduma imefika kwa wakati na karibu na no wajibu waho
kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujiendeleza.
Ukiangalia
masomo haya yanatolewa kuanzia ijumaa mpaka juma pili hivyo hatiaathili
utendaji kazi wetu walisema walimu hao.