MATIKO NITASIMAMIA SHERIA NA FEDHA ZA MIRADI YA WANANCHI.
MATIKO
NITASIMAMIA SHERIA NA FEDHA ZA MIRADI YA WANANCHI.
Mbunge
wa jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Esther Matiko amesema kuwa atahakikisha anasimamia sheria na kanununi na
taratibu za utumishi wa Umma pamoja na fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya
jamii zinazotoka serikali kuu kupitia Halmashauri ya mji wa Tarime mjini kwa
lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hayo
yamebainishwa kipindi akiongea na Cleo News baada ya kutembelea gereza la wafungwa
Wilayani Tarime Mkoani Mara na kutoa misaada mbalimbali kwa lengo la kutatua
baadhi ya changamoto zinazowakabili wafungwa hao na mahabusu.
Mbunge
huyo amesema kuwa kulingana na mazoea ya wananchi wakiwemo watumishi wa umma
pamoja na sekta binafsi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea hivyo alisema kuwa
atahakikisha anasimamia vikali maadili ya utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na
kusimamia ipasavyo fedha za miradi ya wananchi zinzotoka serikali kuu kwa lengo
la kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Mbunge
huyo akiwa jimboni kwake ameweza kutembelea Taasisi mbalimbali likiwemo za Serikali na zisizokuwa za kiserikali huku
akipokea changamoto na baadhi kuzifanyia kazi pia ameweza kutembelea Gereza la
Wilaya ya Tarime na kutoa Msaada wenye thamani ya shillingi 2,144,000 ikiwemo Ng’ombe
mmoja mwenye thamani ya shilingi laki
nne na themanini , computer aina Dell ,
printer HP, chelehani , mchele kilo 257, na mafuta ya kula.
“Nimeamua kutoa msaaada huu kwa wafungwa wa gereza
la Tarime mabalo pia lina watu utoa Wilaya ya Rorya. Serengeti na Tarime
Vijijini na Mjini kwa lengo la kuwapunguzia baadhi ya changamoto lakini bado
nitaendelea kuwasemea Bungeni kama Mbunge wao” alisema Matiko.
Mbunge huyo amewaomba wananchi wake kushirikiana
vyema kwa lengo la kujenga Tarime huku wakiondokana na tofauti za vyama kwani
wakati wa ushabiki wa vyama umeisha bali washirikiane kwa kushirikisha mawazo
ya kuijenga Tarime mjini.