MASABA WANANCHI ENDELEA KUFICHUA WAHARIFU WA MALI ZA UMMA.

PICHA YA SHULE YA MADAWATI KATIKA SULE YA MSINGI MWAMOTO HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI MKOANI SIMIYU.




MASABA WANANCHI ENDELEA KUFICHUA WAHARIFU WA MALI ZA UMMA.

 Wakati serikali ikijitahidi kuboresha elimu  hapa nchini, wananchi wa kijiji cha mwamoto wilayani bariadi mkoani simiyu wamewakamata watu wawili wakiwa na kipande cha dawati  la shule ya msingi mwamoto kufuatia kukithiri kwa wizi wa madawati shuleni hapo ambao umekuwa ukifanyika mara kwa mara hapo nakupelekea  wanafunzi kuendelea kukaa chini wakati wa masomo hivyo wameiomba serikali ili kuunga mkono juhudi za elimu bure kuchukulia hatua kali watuhumiwa hao ili kuweza kukomesha vitendo vya wizi wa mali za umma  kijijini hapo.

Aidha Shule ya msingi mwamoto yenye jumla ya wanafunzi I200 na  hapo awali ilikuwa na madawati 84 ambapo ni madawati 50 tu yanayotumika huku 34 yakiwa yameng’olewa mbao na kubakia vyuma vitupu suala ambalo ni changamoto kubwa kwa wanafunzi na kupelekea kukaachini kwa wanafunzi hao.

Jamboleo  imeshuhudia madawati mengi  ya shule ya msingi ya mwamoto yakiwa yameng’olewa  mbao na baadhi kubakia vyuma tupu ambapo viongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wananchi  na  walimu  baada ya kugundua upotevu huo walifanya mtego na hatimaye kumkamata fundi seremala akiwa na kipande chadawati ambapo amekiri kuletewa na Bw MasukeNdibato  kwaajili ya kutengenezewa benchi  na hivyo wote kufikishwa kwa mtendaji wa kata ya nkololo ,  huku wakiomba sheria ichukue mkondo wake dhidi ya watuhumiwa ili kukomesha wizi uliokithiri shuleni hapo.

Kwa upande mbunge viti maalum mkoa wa simiyu (CHADEMA)Gimbi Masaba amesikitishwa na kitendo hicho cha wizi wa madawati kulingana na juhudi za serikali kuwa elimu bure kwa lengo la kila mtu kupata elimu hiyo hivyo mbunge huyo ameiomba jamii kuzidi kufichua waharifu hao  wanaoiba miundombinu ya serikali ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha mbunge akilaani vikali kitendo hicho alisema kuwa kwa sasa serilikali ya awamu ya Tano kwa kushirikiana na viongozi wote wamejipanga kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu hivyo kama watu wachache wameanza kuiba miundombinu ya serikali hawana budi kuchukuliwa hatua kali kwa lengo la kuhakikisha miundombinu hiyo inakuwa salama.

“Sisi kama wazazi tunajinyima na kuchangia madawati ili wanafunzi waweze kuwa na mazingira rafiki ya kusomea lakini wachache wasiopenda masomo wanaaribu miundombinu na kuiba lazima hatua kali zichukuliwe kwa waharifu hawa ili liwefundisho kwa  wengine” alisema Masaba.

kwa upande wake mtendaji wa kataya Nkololo George Epafra  amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili huku akidai kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa lengo la kukomesha wizi huo wa miundombinu ya serikali katani humo.

Hata hivyo Mtendaji huyo alisema kuwa wizi mbalimbali wa miundombinu ya serikali umekuwa ukiharibiwa vikali katani kwake lakini kulingana na juhudi za wananchi ambazo wameanzakuonesha kwa kuwafichua waharifu hao lazima tabia hiyo itakomeshwa katani humo.

     …..Mwisho….
Powered by Blogger.