WALEMAVU WA NGOZI (ALBINISM) WAMUOMBA MAGUFULI KUSIKIA KILIO CHAO.
PICHA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA SIMIYU AKIKABIDHI MSAADA WA MAFUTA YA KULA KWA MMOJA KATI YA WATOTO WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BIKIRA MARIA. |
WALEMAVU WA NGOZI (ALBINISM) WAMUOMBA
MAGUFULI KUSIKIA KILIO CHAO.
Kutoakana na
matukio ya mauaji kwa wtu wenye ulemavu wa ngozi albino kwa sababu ya imani za
kishirikina, Watoto wanaolelewa katika kituo cha bikira maria kilichopo lamadi Wilayani Busega Mkoani Simiyu
wameiomba serikali ya awamu ya Tano kupitia kwa rais wake Jon Magufuli kukomesha suala zima la mauji ya walemavu wa
ngozi (Albinism) ikiwa ni pamoja na kukomesha suala zima la kutelekeza kwa
watoto wanaozaliwa na ulemavu wa viungo.
Hayo
yamebainishwa jana na watoto wenye ulemavu wa ngozi pamoja na ulemavu wa viungo
wanaolelewa katika kituo cha Bikira Maria kilichopo Lamadi wilayani Busega
Mkoani Simiyu ni kipindi walipotembelewa na mbunge wa viti maaluku mkoani humu
kupitia CHADEMA Gimba Massaba.
Akikabidhi
msaada wa sabuni, Sukari, Mafuta pamoja na juice mbunge huyo alisema kuwa
ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa kuona ni jinsi gani watu hao wamekuwa
wakiishi katika mazingira hatarishi huku wakikosa malezi ya wazazi wao.
“Baada ya
kufika hapa na kuona watoto hao nimeguswa sana kwa kuwa nimechaguliwa
kuwatumikia wananchi na moja kati ya wananchi wa mkoa wa simiyu ni watoto hawa
nitashirikiana na nyie kwa ukaribu kwa
lengo la kuwasaidia” alisema Mbunge.
Hata hivyo
mbunge huyo alisema kuwa ataweza kushiriki chakula cha pamoja na watoto
haoambao wanalelewa katika kaituo cha bikira maria kwa lengo la kuwafariji.
“Na mimi ni
mzazi najua malezi ya mama hivyo kama mzazi na kiongozi wao lazima sikuku
nitashinda hapa pamoja na diwani wangu wa kata ya lamadi wakiwemo viongozi
wengine” alisema Mbunge.
Belensi
Alkard ni mratibu wa kituo hichoi chenye jumla ya watoto 54 alisema kuwa kituo
hicho kinakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio, Vita na
magodoro.
Aidha
mratibu huyo aliongeza kuwa mbali na kuwepo kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi
wapo pia wenye utindio wa ubungo hivyo ameyaomba mashirika mbalimbali kuweza
kuwasaidia watoto hao.
“Suala
ambalo pia ni changamoto na ni lina ghalama kubwa ni mafuta kwa ajili ya kupaka
ngozi za watoto hawa ambao ni albinism” alisema Mratibu
Akitoa
shukrani Mkurugenzi wa kituo hicho Maria Hellena amesema kuwa vituo vya kulelea
watoto yatima , watu wenye ulemavu wa ngozi serikali wamekuwa
wakivitelekeza huku akitoa mwito kwa
jamii pamoja na serikali za vijiji,
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa watu kwa kutambua umuhimu wa walemavu wa aina yeyote na
watoto yatima wamekuwa wakianzisha vituo
lakini jamii ianatelekeza watoto wao pale wanapopelekwa kwa ajili ya kulelewa
suala ambalo ni chanagamoto kubwa kwani watoto hao mbali na kulelewa nje ya
familia wana haki ya kutambua wazazi wao.
Bas
Kreakuiet kutoka Nchini uolanzi ni kati ya watu ambao wamejitoa kusaidia kituo
hicho akitoa msaada wa mafuta katika
kituo hicho alisema kuwa anaguswa sana na ndiyo maana ameamua kusaidia mafuta
bure kwa kutumia ghalama zake huku akitoa mwito kwa serikali ya Tanzania
kuingilia kati suala zima la mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
,,,,,,MWISHO….