MBUNGE WA VITI MAALUMU VIONGOZI ONDOENI TOFAUTI.
MBUNGE WA VITI MAALUMU VIONGOZI
ONDOENI TOFAUTI.
Mbunge wa
viti maalumu mkoa wa Simiyu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA Gimbi Massaba amewataka viongozi
wa chama hicho kuondoa tofauti walizonazo kwa lengo la kujenga chama ikiwa ni
pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka.
Hayo
yamebainishwa katika ziara yake ya kibunge ambayo inaendelea Mkoani Simiyu kwa
lengo la kuzungumza na viongozi wa chadema wilaya ili kuweza kuondoa
taofautizilizojitokeza kwa baadhi ya viongozi katika uchaguzi uliopita.
Akiongea na
Wenyeviti wa wilaya, Makatibu Wilaya, Wenezi, Wilaya na majimbo kutoka katika
mkoa mzima Wilayani Busega mbunge huyo alisema kuwa kwa sasa viongozi hao
hawana budi kuondokana na tofauti kwani uchaguzi umemalizi bali wakae kwa
pamoja na kushirikiana kwa lengo la kujenga chama upya huku wakitekeleza ahadi
za wananchi walizowahaidi kipindi cha kampeni.
“Sote
tunatambua kuwa tulishirikiana
kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa lengo la kuongoza serikali na Halmashauri
zake zote, Tulipambana kila mmoja, Wengine wameumia na kupotea maisha yao na
kuacha family yatima na baadhi wakipata ulemavu wa kudumu kwa lengo la
kupigania chama hivyo wakati umefika tukaunganishe nguvu ili kujenga simiyu
upya” alisema.
Hata hivyi
mbunge huyo alisema kuwa ni wakati
sasa viongozi hao ngazi ya wilaya na
mkoa kuhakikisha wanachukua hatua
stahiki bila kumwonea mtu yeyote anapobainika kafanya kosa kinyume na katiba,
kanuni na maadili ya chama hicho ili kuendelea kulinda heshima ya chama.
Aidha
Massaba alitoa mwito kwa viongozi
kujenga utaratibu wa kuhudhuria vikao vya maendeleo ya kata na mabaraza
ya madiwani ili kuweza kufaamu vitu vinavyozungumziwa huku wakijenga hoja na
kuwapeleakea wananchi katika mstakabari wa maendeleo.
“Mimi kama
mbunge wenu nitaendelea kushirikiana
nanyi vyema katika ujenzi wa chama kwa kutumia mshahara wangu ikiwa ni pamoja
na kuhakikisha tunafanya vizuri katika uchaguzi ujao” alisema.