TARIME WAFANYA MAAMUZI KUCHAGUA KIONGOZI MWANAMKE MARA YA KWANZA,TARIME WAONDOKANA NA MFUMO DUME

    

Kulingana na mfumo dume ambao umekuwa ukimukandamiza Mwanamke katika uongozi umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kumunyima mwanamke nafasi ya uongozi na wakati mwingine kukosesha Maendeleo katika eneo huska kwani tumekuwa tukiona maeneo ambayo yanaongozwa na wanawake yamekuwa endelevu hata kuzidi maeneo yanayoongozwa na wanaume.

Mkoa wa Mara Wilayani Tarime katika jamii ya Kikurya wamekuwa wakiamini kuwa Mwananmke hawezi kuongoza kulingana na Mgumo dume na Mila potofu ambazo wamekuwa wakiamini jambo ambalo siyo kweli lakini baada ya kutolewa kwa Elimu za kiraia kupitia mbalimbali ya Kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali Makanisani, Mikutano ya hadhara na Mashuleni jamii imeweza kubadilika na kuanza kumwamini mwanamke kuwa anaweza kuwa kiongozi Mzuri.

Esther Matiko ni kati ya Mwananmke pekee ambaye ameweza kudhubutu na kuwania ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambapo mwana mama huyo ameonekana kukubalika katika jamii pasipo kuingiza mfumo dume ambao umekuwa ukikandamiza mwanamke hapo awali na mwanamke huyo ameonekana kuwa na nyota ya kungaa katika kipindi chote cha kampeni suala ambalo limeweza kumpa ushindi mkubwa na kuweza kuwa mbunge wa Jimbo la Trime mjini kwa ushindi wa kura 20017 dhidi ya Mgombea mwenzake kutoka chama cha Mapinduzi Michael Kembaki kwa kura14025.

Kutokana na mfumo kandamizi ambao ulikuwa ukiwakandamiza wanawake mwanamke hakuwa na nafasi yeyote katika suala zima la uongozi lakini baada ya jamii kupata elimu ambazo zimeka\uwa zikitolewa na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali matokeo yake tayari mkoa wa Mara umeweza kupata wabunge wa kike wawili Esther Matiko jimbo la Tarime Mjini na Esher Bulaya Jimbo la Bunda Mjini wote kutoka vyama vya upinzani ambavyo vinaundwa na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.

TGNP Mtandao ni kati ya Shirika moja wapo kwa kushirikiana na Mashirika mengine kikiwemo Chama cha waandishi wa Habari wanawake (TAMWA) wamekuwa mstari wa mbele kupaza sauti kwa ajili ya kudai hakiza mwanamke jambo ambalo limeweza kuzaa matunda katika uchaguzi wa mwaka huu hivyo haeana budi kupewa shukrani zao kwani wamekuwa mstari wa mbele kupigania mwanamke
 
"Jamii nyingi imeweza kubadili mitazamo hasi katika nyanja zote japo katika maeneo tofauti bado mwanamke anakakandamizwa na mfumo dume  na lengo letu ni kuhakikisha tunapambana na kumkomboa mwanamke wa Taifa hili ni moja ya kauli ambayo ilishawahi kutumiwa na mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liund"
Matiko ambaye ni mgombea Ubunge kupitia CHADEMA ambaye pia alikuwa akichuana na wabunge wawili mmoja kutoka Chama cha ACT Wazalendo ambaye alipata kura 356 na Chama cha Mpinduzi Michael Kembaki kura 14025 huku mwana mama huyo akijinyakulia kura 20017 nakuibuka mshindi katika jimbo la Tarime Mjini.

Akiongea jamboleo baada ya kuibuka mshindi na kutangazwa rasmmi na msimamizi wa uchaguzi Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Tarime Juma Mwajombe Matiko alisema kuwa kwa sababu waananchi wa Tarime wamemuchagua nakuweza kumwamini kama mwanamke ni kuhakikisha analeta maendeleo kupitia kata Nane zinazounda jimbo la Tarime Mjini.

 "Katika kampeni zangu nimeweza kudhalilishwa katika majukwaa kwa sababu ya jinsia yangu lakini mwenyezi mungu ametenda maajabu na wanatarime sasa mmedhihilishia umma kuwa suala zima la mfumo dume limeondoka naamini sitawaangusha binti yenu" alisema Matiko.

Jimbo la Tarime mjini ambalo ni jimbo jipya linaundwa na kata Nane ambazo ni Nyamisangura, Sabasaba, Bomani, Kitare, Nyandoto, Turwa, Kenyamanyori, na Nkende hivyo mbunge huyo alisema kuwa atahakikisha anatimiza ahadi alizozitoa katika kipindi chake cha kampeni kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ususani Sekta ya Maji, Elimu,Miundo mbinu ya Barabara  pamoja na Afya,

                                                      ..   .......MWISHO.....




Powered by Blogger.