PICHA YA MBUNGE MTEULE WA JIMBO LA TARIME MJINI ESTHER MATIKO AKIKABIDHIWA HATI YA USHINDI NA ALIYEKUWA MSIMAMIZI MKUU WA UCHAGUZI JIMBO LA TARIME MJINI KAIMU MKURUGENZI JUMA MWAJOMBE Mbunge mteule wa jimbo la Tarime mjini kupitia chama cha Demkokrasia na maendeleo CHADEMA Esther Matiko amekabidhiwa rasmi hati ya Ushindi wa jimbo hilo huku akisema kuwa ataenda kutekeleza ahadi zote ambazo aliweza kuhaidi katika kipindi chake chote cha kampeni. Mbunge huyo alisema kuwa katika wilaya ya Tarime Mjini inakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma ya Maji Elimu pamoja na Huduma ya Afya hivyo amesema kuwa ataenda kutatua changamoto hizo kwa lengo la kuleta maendeleo kwa watanzania wote bila kubagua itakadi ya vyama. Aidha Mbunge huyo alisema kuwa atahakikisha fedha kutoka Serikali kuu atahakikisha zinawafikia wananchi wote kwa lengo la kufanya maendeleo ili kuweza kuwaondolea wananchi changamoto hizo. "Kwa ushirikiano ambao naenda kupewa na madiwani kwa sababu Halmashauri tayari inaenda kuundwa na chadema na kwa kuwa wanatarime wameweza kuniamini na kuweza kuandika historia ambayo haijawahi kuwepo dunia hii sasa naenda kuonesha ushujaa wangu" alisema Esther. Mbunge huyo mtehule alisema kuwa wanatarime wamefanya tukio la kihisoria ambal halijawahi kuwepo tangu dunia kuwepo hivyo mbunge huyo amehaidi kutimiza ahadi zote ambazo aliweza kutoa katika kipindi chake chote cha kampeni. Esther Matiko alishinda kwa kura20017 dhidi ya Mgombea mwenzake kutoka chama cha Mapinduzi Michael Kembaki kwa kura14025 nakuweza kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa Tarime mjini ambalo ni kati ya Jimbo jipya kati ya majimbo mapya ambayo yalitangazwa. Hata hivyo Esther Matiko ni Mwanamke wa kwanza kuongoza jimbo hilo kulingana na mila potofu za kabila la kikurya walikuwa wakiamini kuwa mwanamke hawezi kuongoza lakini itadhilisha kuwa mwanamke anaweza kuongoza vyema kuliko hata wanaume. .......Mwisho.....
|