WANAWAKE WAITAKA SERIKALI ITAKAYOCHAGULIWA KUTOA VIPAUMBELE KWA MAKUNDI YOTE.

Ni picha ya mkurugenzi mendaji wa TGNP Mtandao Bi: Lilian Liund akizungumza katika ufunguzi wa tamasha la uzinduzi wa ilani ya uchaguzi  ya mtandao wa wanawake na katiba na uchaguzi.
WANAWAKE WAITAKA SERIKALI ITAKAYOCHAGULIWA KUTOA VIPAUMBELE KWA MAKUNDI YOTE. 

Wananwake wameitaka Serikali itakayo ingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu iwe na jukumu la kusawazisha uwanja wa ushindani huku ikiweka utaratibu wa kwa wagombea wanawawake ,vijana ,pamoja nawatu wenye ulemavu ili waweze kunufaika na rasilimali za uchaguzi huku wakiomba Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kudhibiti na kupambana na rushu pia wakiitaka tume ya uchaguzi kusimamia vyema kanuni na maadili ya uchaguzi ambazo vyama vya siasa zimelidhia ili kuwe na uchaguzi ulikuwa uhuru unaozingatia haki nausawa wa jinsia.


Hayo yamebainishwa  hii leo na na mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tamwa BI Edda Sanga katika  uzinduzi wa tamasha la uzinduzi wa  iliani ya uchaguzi ya mtandao wa wanawake na katiba ya uchaguzi jijini Dar es salaam.


Bi Senga amesema kuwa wao kama wanaharakati wamekuwa wakipaza suati zao kwa lengo la kumkomboa mwanamke na hivyo wameitaka serikali itakayoingia madarakani kuangalia vipaumbele vya mwanamke vijana na watu wenye ulemavu.

 Kwa upande wake  Mwenyekiti wa  Bodi ya Chuo cha  mafunzo ya jinsia (GTI) ambaye pia ni mwananchama wa TGNP mtandao  Mama Asseny Muro akieleza lengo la ilani  hiyo amesema kuwa wanawake ndo nguzo ya taifa kwani bila mwanamke haku a maendeleo hivyo lengo lao ni kupaza sauti huku wakishiriki kikamilifu katika uchaguzi huku akisema kuwa wanawake ni zaidi ya asilimia 51 ya wananchi wa Nchi hii.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Mtandao Bi: Lilian Liundi amesema kuwa watahaikisha wanatengeneza mikakati kwa lengo la kuondoa Mifumo kandamizi kwa mwanamke.
Tamasha hili limefunguliwa hii leo katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam na kumalizika Septemba 4 huku zikijadiliwa mada mbalimbali kuhusu Uchaguzi uliopo hapo mbeleni ikiwa ni pamoja na kuzungumzia vitendo vya ukatili na mafanikio ya matamasha hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.
                                                         MWISHO....
Powered by Blogger.