MATIKO AWASILISHA MAPINGAMIZI MAWILI.

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Mara CHADEMA Esther Matiko  ambaye pia  anawania jimbo la Tarime Mjini akiwasilisha mapingamizi ya Chama cha ACT Wazalendo na Chama cha Mpinduzi (CCM) katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime.
                                              Tarime.

CHADEMA WAMTAKA MKURUGENZI KUSIMAMIA HAKI KATIKA UCHAGUZI,
MATIKO AWASILISHA MAPINGAMIZI MAWILI.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilayani Tarime Mkoani Mara kimemwomba Mkurugenzi wa Halamashauri ya Mji wa Tarime Venance Mwamengo ambaye ni msimamaizi  mkuu wa Uchaguzi kusimamia haki katika uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais uanaotarajia kufanyika October 25 mwaka huu huku  viongozi wa Chama Cha Mapinduzi amabo wako serikalini kuondokana na suala la  kuwatumia vibaya watumishi wa Halmashauri mbalimbali kwa kwa sababu ya Maslahi yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara CHADEMA Esther Matiko ambaye pia anagombea jimbo la Tarime Mjini kipindi alipokuwa akiwasilisha mapingamizi ya wagombea wawili akiwemo  Mgombea wa chama cha ACT Wazalendo Deogratias Meck na Anayegombea kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi wote jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki.

Akiongea na ns gazeti hili  Esther matiko alisema  kuwa Wakurugenzi ambao ni wasimamaizi wakuu wa uchaguzi wamekuwa wakienda tofauti na sheria na kanuni za uchaguzi zinavyosema suala ambalo linaweza kusababisha machafuko kuwa chama hicho hakitaki amani kutoweka bali wakurugenzi wasimamie haki na qwananchi wako tayari kuchagua kiongozi anaye wafaa na siyo kuchaguliwa .

 Aidha Matiko ameongeza kuwa baadhi ya viongozi ambao wamewekwa na chama cha Mapinduzi wamekuwa wakiwanyanyasa watumishi wa Halmashauri za Wilaya na Miji kwa sababu ya Maslahi yao binafsi suala ambal CHADEMA haitakubaliana nalo.

"Watumishi wa Umma wamekuwa wakitumiwa vibaya na viongozi wanatokana na chama cha mapinduzi na kufanya maamuzi ambayo hawakuyatarajia sasa katika uchaguzi wa mwaka huu lazima hili tulifanyie kazi hakuna cha goli la Mkono hapa" alisema Matiko.


Matiko aliongeza  kuwa amewasilisha Mangamizi mbili kwa chama cha ACT Wazalendo ambacho mgombea wake ni Deogratias Meck ambaye amekiuka taratibu takribani tano likiwemo la  la Mhuri wamahakamu kuhusu Tamko lake, na Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Michael Kembaki akiwa na pingamizi moja la kisheria kuhusu Udhamini.

Matiko alisema kuwa alipeleka pingamizi hilo kuanzia majira ya saa tisa nakukuta Ofisi za Halmashauri ya mji zikiwa zimefungwa na kuamu kuwapigia wasimamizi wakuu wa uchaguzi ngazi ya Taifa na kukemea suala la kufungwa kwa ofisi kabla ya mda hususani katika kipindi tunachoelekea cha uchaguzi.



.......Mwisho......
Powered by Blogger.