Mkuu wa Mkoa anzisheni mradi wa kufuga kuku wa kienyeji ili kuondokana na umaskini
Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Asser Msangi akiongea na wananchi wa kijiji cha Mirare wilayani Rorya Mkoani Mara ambao wamenufaika na mfuko wa jamii TASAF III katika kuudumia kaya Maskini.
Mkuu wa mkoa wa Mara Asser Msangi amewataka wananchi wanaotoka katikam kaya maskini kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa Kienyeji kwa lengo la kujiongezea kipatao kutokana na frdha wanazopewa na Mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAFkwa ajili ya kunusuru kaya Maskini.
Kauli hiyo imetolewajana katika vijiji vya Mirare na Nyamasanda wilayani Rorya Mkoani Mara kipindi Mkuu wa mkoa alipokuwa akiongea na wananchi wanatoka katika kaya Maskini huku akitoa elimu jinsi gani wanufaike na fedha wanazopata kutoka katika mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF III katika mpango wa kunusuru kaya maskini.
Mkuu wa MKoa alisema kuwa fedha zinzotolewa kwa wananchi ni chache kulingana na mahitaji hivyo hawanabudi kuanzisha miradi midogomidogo ikiwemo ufugaji wa kuku wa kienyeji pamoja na bihashara ndogondogo huku wakijifunza kutunza akiba kulingana nafaida wanayoipata ili baada ya miaka mitatu mradi huo utakapmalizika waweze kijikimu kwa kuondokana na uaskini.
"Kila mwananchi nina uhakiki anauwezo wa kufuga kuku endapo ataweza kupewa Elimu ya kutosha na baada ya mwaka mmoja kuku hao lazima wataongezeka na kuwaondolea umaskini" alisema Mkuu wa Mokoa.
Aidha Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa ili wananchi wa Rorya waondokane na umaskini hawana budi kuanzisha kilimo cha Matunda kama vile Zabibu,Maembe na Machungwa pamoja na kilimo cha Mihogo ambayo inakinzana na ugonjwa ambao kwa sasa wananchi wamedai kuwa mihogo inashambuliwa na ugonjwa.
Akisoma taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa Mara Mkurugenzi wa Halmashauri Wilayani Rorya Mkoani Mara Charles Chacha alisema kuwa kuwa katika zoezi la utambuzi wa kaya maskini kaya7,724 zilitambuliwa ikiwa ni asilimia 98 ya kaya 7811 zilikuwa zimelengwa.
Aidha Mkurugenzi alisema kuwa jumla ya kaya 7,360 ziliweza kupokea fedha kiasi cha shilingi 273,188,000 kati ya kaya 7,366 ambazo zililengwa kupokea kiasi cha shilingi 273,448,000 hivyo kaya 6 kati ya kaya7, 366 hazikuchukua fedha kiasi cha shilingi 260,000 ambapo zilirudishwa TASAF Makao makuu.
Hata hivyo Chacha alizitaja changamoto kuwa ni zipo familia nyingi zinazojilinganisha kuwa kaya maskini lakini hazikufanikiwa kuingia katika mpango wa kunusuru kaya maskini,
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyamasanda Bi Veronica Jemsi akisoma taarifa alisema kuwa baada ya malipoa hayo utoro utapungua shuleni huku watoto wakipelekwa kliniki na kuboreka kwa rishe.
Kwa Upande wake Mkuu wa wilaya ya Rorya Felix Lyaniva alisema kuwa wataweka mpango mkakati wa kuanzisha kilimo cha m,atunda kulingana na agizo la mkuu wa mkoa kwa lengo la kukuza uchumi wilayani humo huku wakitoa ajili za kwa vijana.
"Nataka baada ya miaka miwili wakazi wa rorya wanaulize soko la kuuza mihogo kwani mikakati niliyonayo lazima tuanzishe kilimo bora chenye tija ikiwa ni pamoja na kupanda mbegu zinzokinzana na ugonjwa" alisema Mkuu wa Wilaya.
; ....... Mwisho.....